SPIKA NDUGAI AWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI KUSIMAMIA RASILIMALI ZA TAIFA

 


📌DOTTO  KWILASA

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amewataka Viongozi wa Serikali kusimamia vyema rasilimali za Taifa kwa kuzingatia misingi ya uongozi na kuwatumikia wananchi bila ubaguzi.

Ndugai ameyasema  hayo wakati akifunga Mkutano wa  Mafunzo ya Uongozi ya  siku nne kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi.

Akiongea katika mkutano huo amewashauri Wakuu wa Mikoa na Makatibu tawala kuacha kulewa  madaraka na  badala yake watumie uongozi wao kusimamia miradi ya maendeleo na kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia kanuni na sheria.

Licha ya hayo amesema  ni vyema Viongozi hao  wakafanyie  kazi  mafunzo hayo kwa kuepuka majivuno na kuwanyanyasa walio chini yao bali kutenda haki kwa   bila kujali maskini au matajili huku  wakizingatia miiko ya uongozi na mipaka ya kazi yao huku akisisitiza kuwa cheo ni dhamana.

 Nawapongeza kwa kuteuliwa na kushika nafasi si jambo dogo, ninyi mmeanza na awamu ya sita chini ya Rais Samia msilewe madaraka kumekuwa na kasumba kwa viongozi wengi wanalewa madaraka wanapigiwa simu hawapokei, mmepewa dhamana ya kumsaidia Rais katika mkoa sasa ukiwa hupatikani unategemea nini,amesema na kuongeza;

Kasimamieni sana shughuli za maendeleo na bajeti ya serikali, na maendeleo  ya watu wenu kuanzia ngazi ya kaya na familia kwani  maendeleo ya wananchi hayawezi kuja yenyewe yatatokana na ubunifu wenu na imani yenu kwao

Spika Ndugai.

Spika Ndugai pia amewashauri wateule hao Kujihusisha na masuala ya kilimo kwani kuna aina na mifumo mingi ya kufanya au kuendesha shughuli hiyo kwa njia ya kisasa na kupata kipato kinyume na Kilimo kilichokuwa kinafanyika zamani.

"Kilimo chetu kimekuwa chenye tija na Kilimo cha kuzoeleka kimeanza kupotea sasa mkaweke nguvu kusukuma gurudumu hili lifike mahali panapo stahili,

 Kiongozi mzuri akiongea ,watu humsikiliza ,mkianza ninyi kama mfano na wananchi mnaowangoza itakuwa rahisi kuwaelekeza kwa vitendo, Lazima ninyi mkajenge   misingi inayotakiwa ili wananchi wenu wapate maendeleo kupitia kilimo, mifugo uvuvi na huku ninyi mikiwa  mstari wa mbele kuzifanya shughuli hizo,"amesema

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu amesema mafunzo yaliyotolewa na taasisi ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala yatawasaidi kuboresha utendaji kazi wao na kuijenga Tanzania mpya.

Alisema   mafunzo hayo yamechukua siku nne kwa wakuu wa mikoa 26 na yamegusa sehemu za msingi ambazo zitawasidia katika maeneo yao ya kazi na kuimarisha uhusiano kati ya viongozi wa mkoa na wale wa kitaifa

"Niwapongeze Sana taasisi ya uongozi kwa kuandaa mafunzo ambayo naamini yataleta chachu ya mabadiliko kwa wakuu na mikoa katika maeneo yao ya kazi pia nawapongea wakuu wa mikoa kwa kuonyesha ushirikiano  kuanzia siku ya kwanza hadi mafunzo yalipofika tamati" alisema

Kwa upande wake Mwakilishi wa Taasisi ya Uongozi Zuhura Muro amesema hadi sasa  taasisi hiyo imeweza  kuwafikia viongozi zaidi 7000 wakiwemo wakuu wa mikoa, matibu tawala na watendaji wa halmashauri.

Kutokana na hatua hiyo ameipongeza Ofisi ya utumishi wa Umma kwa  kuwezesha mafunzo hayo  kwani ni sehemu ya maagizo yaliyotolewa na waziri  Mohmed Mchengelewa ambaye aliiagiza  taasisi kuwafikia viongozi wa umma . 

"Mafunzo haya ya wiki nzima yamepata fursa ya kutoa mada 10 ambazo ni  uongozi binafsi, itifaki, maadili ya uongozi na rushwa, usuruhishi wa migogoro, muundo wa serikali kuu, mahusiano yenye Tija, mahusiano ya kisekta, usimamizi Fedha, usimamizi wa miradi na usimamizi wa rasilimali za umma,

Ameongeza kuwa "Tunaishukuru TAMISEMI kwa kuona umuhimu na kuwezesha mafunzo haya kwa kada hii muhimu na wizara zote zilizofika na kutoa mafunzo mbalimbali ya kisekta ambayo yataleta mabadiliko makubwa kwenye utebdaji," alieleza

Akitoa neno la shukurani Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martini Shigela alisema wanamshukuru Rais Samia kwa kuwaamini na kuwapa nafasi miongoni mwa wengi na kumuhakikishia kuwa watawatumikia wananchi 

"Nawapongeza washiriki kwa kuonyesha moyo na dhamila ya kujifunza kwani toka mafunzo haya yaanze kila mshiriki alikuwa anashiriki kwa asilimia zote, na kutokana na mafunzo haya tunaahidi kuyatekeleza yote na kati yetu hakuna jambo baya litajitokeza miongoni mwetu,"amesema.

 

Post a Comment

0 Comments