DODOMA YA MAANDALIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI

 


📌DOTTO KWILASA

OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu imewakutanisha  viongozi wawakilishi wa Serikali ngazi mbalimbali,makundi ya kijamii ,Taasisi za dini,Umma ,binafsi na vyama vya siasa katika kikao cha pamoja kwa lengo la uhamasishaji na utoaji wa elimu ya sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwaka 2022 .

Akieleza umuhimu wa kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka amesema wameandaa kikao hicho na kuyashirikisha makundi hayo ili kurahisisha utoaji wa elimu ya sensa kwa jamii huku akisisitiza kwamba kwa kufanya hivyo zoezi hilo litafanikiwa kama inavyotarajiwa.

Kwa kutambua umuhimu wa zoezi hilo, Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene  amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika zoezi  la  sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika mwakani  ili kuiwezesha Serikali kupanga maendeleo na kukuza uchumi.

Akiongea katika  kikao hicho amesema

Serikali inategemea sana zoezi hili,hatuwezi kuwa na maendeleo bila kujua idadi ya watanzania,kila mmoja kwa nafasi yake anatapaswa kuwa balozi wa uhamasishaji  ni muhimu hivyo watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi ili kuisaidia Serikali kupanga mipango ya maendeleo

Mbali na hayo ametumia nafasi hiyo kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Antony Mtaka  kwa kuona haja ya kuandaa mkutano huo huku akisisitiza kwamba sensa ni muhimu kwani inaleta ushahidi wa kisayansi na maendeleo.


Naye Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Kongwa,Job  Ndugai amesema zoezi hilo ni muhimu kwa Taifa kwani litasaidia Nchi kupanga maendeleo hivyo watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.

Tarehe 31 vikao vyetu vya Bunge vitaanza na vikao vilivyopita tumepitisha mambo mengi ikiwemo na tozo,safari hii itakuwa salama,hili ni jambo muhimu sana hivyo niwaombe watanzania wajitokeze kwa wingi,sisi wagogo hata zoezi la kuhesabu mifugo linakuwa na shida
ni utamaduni wetu.

Naye Kamisaa wa Sensa nchini ambaye pia ni Spika wa Bunge Mstaafu,Anne Makinda ametoa wito kwa watanzania kujitokeza katika zoezi la kuhesabiwa kwani hilo sio suala la kisiasa na kwamba  zoezi hilo watatumia tehama katika maeneo ya kuhesabiwa lengo likiwa ni kuwafikia watanzania wengi ambapo amedai watawafikia watu wengi mpaka katika maeneo ya vijijini.

Post a Comment

0 Comments