NBS YAELEZA UKUAJI WA UCHUMI ROBO YA KWANZA KWA MWAKA 2020

 


📌DOTTO KWILASA

KAIMU Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel Masolwa amesema katika kipindi cha robo ya kwanza (Januari-Machi)Mwaka 2021,pato la Taifa kwa bei za miaka husika liliongezeka hadi Shilingi trilioni 38.0 kutoka Shilingi trilioni 36.4 katika kipindi kama hicho Mwaka 2020

Masolwa amezungumza hayo jana Jijini hapa wakati akiongea na Waandishi wa habari kuhusu ukuaji wa uchumi,robo ya kwanza kwa mwaka 2021.

Alisema,pato la Taifa kwa bei za mwaka 2015 liliongezeka hadi Shilingi trilioni 33.2 katika robo ya kwanza ya mwaka 2021 kutoka Shilingi  31.7 katika kipindi cha Januari-Machi  kwa mwaka 2020 sawa na ukuaji wa Asilimia 4.9.

Akizungumzia ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika kipindi cha robo ya Mwaka 2021,alisema shughuli za uchimbaji wa madini na mawe iliongoza kwa kuwa na kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa asilimia 10.2 ikifuatiwa na Habari na mawasiliano kwa asilimia 9.1.

Kiwango cha ukuaji wa shughuli za uchukuzi na uhifadhi mizigo ni asilimia 9.0,maji safi na maji taka asilimia 9.0 ,huduma za kitaalamu,Sayansi na Ufundi asilimia 7.8 huku huduma zinazohusisana na utawala kwa asilimia 7.4 na umeme asilimia 7.2

Licha ya hayo Kaimu mkurugenzi huyo wa Takwimu za uchumi alisema mchango wa shughuli kuu za kiuchumi kwa kuzingatia mchanganuo wa shughuli kuu za kiuchumi za msingi na shughuli za huduma zinaonyesha kuwa shughuli za huduma zilichangia asilimia 40.1 ya Pato la taifa zikifuatiwa na shughuli za msingi kwa asilimia 37.1 na shughuli za kati asilimia 22.7.

Pamoja na mambo mengine Masolwa alisema,ukuaji wa pato la Taifa katika robo ya kwanza ya mwaka 2021wa asilimia 4.9 ulichangiwa na shughuli zote za kiuchumi zilizofanyika nchini huku mchango mkubwa katika ukuaji ulitokana na shughuli za kiuchumi za ujenzi kwa asilimia 14.9,uchukuzi na uhifadhi wa mizigo kwa asilimia 14.6,kilimo kwa asilimia 12.7 na uzalishaji viwandani kwa asilimia 9.8.

 "Ukokotoaji wa Pato la Taifa umezingatia matakwa ya Mfumo wa umoja wa mataifa wa kutayarisha Takwimu za pato la Taifa unaojulikana Kama system of National Accounts 2008 kwa lengo la kutayarisha Takwimu linganifu kati ya nchi moja na nyingine,"alisema.

 

Post a Comment

0 Comments