CCM YAAGIZA NFRA KUNUNUA TANI 100,000 ZA MAHINDI NYANDA ZA JUU KUSINI

 

📌DOTTO KWILASA

KUTOKANA  na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) Hivi karibuni kudai kuwa kutakuwa na upungufu wa mvua msimu ujao wa kilimo,Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeiagiza Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa  Hifadhi ya Chakula (NFRA)  kununua tani 100,000 za mahindi katika Mikoa ya Nyanda za juu Kusini kuondokana na Uhaba wa chakula.

Hatua hii imekuja  wakati ambapo  tayari  Serikali imekwishanunua tani 24,000 kiasi ambacho kimeelezwa Kuwa ni kidogo na kwamba hakiwezi kukidhi mahitaji ya Wananchi.

Hayo yamebainishwa  leo Septemba 6,2021,na Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo wakati akiongea na Waandishi wa habari huku akifafanua kuwa  mwezi wa saba Sekretarieti ya Chama hicho ilifanya ziara katika Mikoa ya Rukwa,Songwe na Mbeya ambapo walikutana na changamoto ya wakulima kukosa soko la zao la mahindi.

Amesema mara baada ya ziara hiyo waliiagiza Serikali kununua mahindi hayo ambapo  ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 14 ambazo zilinunua zaidi ya tani 24,000.

Amedai  kwa
sasa fedha hizo  zimeisha na wakulima wanaendelea kuhangaika kutafuta soko  la  kuuzia mahindi yao

Kutokana na hali hiyo Katibu Mkuu huyo ameiagiza Serikali kutoa tena fedha na inunue tani 100,000 za wakulima hao kwani wanazotaarifa kwamba msimu ujao wa kilimo mvua zitakuwa chache.

 Tena kwa bei ile ile ya shilingi 500 kwa kilogramu na wafanye zoezi hilo liwe endelevu kwani mamkala ya hali ya hewa imesema kuna changamoto katika mvua za vuli mpaka katika mvua za masika hivyo kutakuwa na changamoto ya upatikanaji wa chakula

Pia amesema katika ziara hiyo wamejifunza kwamba uchache wa vituo vya kununulia mahindi hivyo ameiagiza NFRA kuweka vituo ambavyo vitakuwa karibu na wakukulima.



Kuna malalamiko kukatwa  fedha katika shilingi 500 tunasema hapana mtu aliyepo Mufindi,Ileje,Mbozi,Nkasi  tunataka bei ya mahindi iwe moja kwa wote wa karibu na mbali

Katika hatua nyingine,Katibu Mkuu huyo ameziagiza  Wizara za Kilimo na Fedha na Mipango wakutane kujadiliana jinsi ya kupunguza bei ya mbolea kutokana na kuwa juu hivyo kumuumiza mkulima.

 Amesema kwa sasa bei ya mbolea aina ya Urea imepanda maradufu kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona ambapo awali ilikuwa shilingi 50,000 mpaka 55,000 lakini kwa sasa ni shilingi 80,000 mpaka 85,000.

Post a Comment

0 Comments