IJUE IDADI YA WANAFUNZI WANAOANZA MITIHANI LEO

 


📌NTEGHENJWA HOSSEAH (TAMISEMI)

 

WANAFUNZI Takribani 1,132,143 waliosajiliwa kutoka katika shule za Msingi 17,585 za Tanzania Bara wameanza mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi. Kati ya hao wavulana ni 547,502 sawa na asilimia 48.36 na wasichana ni 584,641 sawa na asilimia 51.64

Kati ya Watahiniwa 1,132,143 waliosajiliwa watahiniwa 1,079,943 sawa na asilimia 95.39 wanafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 52,200 sawa na asilimia 4.61 wanafanya mtihani kwa lugha ya Kingereza.

Aidha watahiniwa wenye mahitaji maalumu  wapo 3,327, kati yao 108 ni wasioona, 951 wenye uoni hafifu,739 wenye uziwi, 358 ni wenye ulemavu wa akili na 1,171 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwilini.

Kwa mwaka 2020 idadi ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 1,023,950 hivyo kuna ongezeko la jumla ya watahiniwa 108,193 sawa na asilimia 10.57 kwa mwaka 2021 ukilinganisha na mwaka 2020

Mitihani hii inalenga kuwapima uwezo na uelewa  wananfunzi katika yale yote waliyojifunza kwa kipindi cha miaka saba.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania Dkt. Charles Msonde.

Post a Comment

0 Comments