MTAKA ATAKA TCB KUONESHA WANAWAKE FURSA

 


 

📌LUCY NDALAMA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka ameitaka   Benki ya Biashara Tanzania (TCB) kuwaonesha wanawake na  kuzifuata fursa ambazo zipo katika maeneo mbalimbali na kisha kutoa fedha kwa  wajasiamali wanawake   ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza leo Septemba 8,2021 wakati wa uzinduzi wa kongamano la wanawake na biashara ambalo liliandaliwa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) Mkuu huyo wa Mkoa ameitaka Benki hiyo kuzifuata fursa mbalimbali na kisha kutoa fedha kwa wanawake ili waweze kujiongezea kipato kupitia fursa hizo.

Katika kongamano hilo wanawake wajasiriamali walipata fursa ya kuifahamu TCB ambapo pia ziliwasilishwa mada mbalimbali ikiwemo nafasi ya mwanamke katika kukuza uchumi wa Taifa,ambapo jumla ya washiriki 350 hasa wanawake walishiriki

Hapa nitawaleta watu wanaojenga Standard Gauge,Tarura na wale wa Bomba la Mafuta waje waseme fursa kwao zipo katika maeneo yapi halafu nyinyi muwape fedha wanawake ili ikiwezekana wasambaze vyakula katika miradi hii

Aidha,amesema changamoto kubwa kwa wanawake ni kukopa mikopo umiza lengo likiwa ni kufanikisha ndoto zao ambapo amedai jambo hilo limekuwa likiwarudisha nyuma hivyo Benki hiyo inatakiwa iwasaidie wapate mikopo yenye riba nafuu.

"Mkurugenzi Mtendaji  tafuta ‘position’ ukijikita kwa wanawake benki yako itakuwa kubwa,hawa wanawake unaowaona hapa wanakopa shilingio 500,000 marejesho shilingi milioni 2 au nakosea(wanashangilia) wasaidieni hawa wajasiriamali kutoka kwenye mikopo umiza,”amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

Pia,amesema jukwaa la wanawake na biashara linaendana na mpango wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika kushiriki na kusimamia uchumi wa Taifa.



Kwa upande wake,Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB,Sabasaba Moshingi amesema atashirikiana na Mkuu wa Mkoa kuhakikisha wazifuata fursa hizo ikiwemo kwenda katika baadhi ya Mikoa.

Hata hivyo, amesema benki hiyo inawajibu kuupa kipaumbele uwekezaji wa wanawake na maendeleo yao baada ya Serikali kuziunganisha shughuli zake na zile za iliyokuwa Benki ya wanawake Tanzania.

Amesema lengo la kongamano hilo ni kuwakusanya wanawake ili waweze kujadiliana kwa pamoja jinsi ya kukuza biashara zao na kuweza kufanikiwa katika maisha yao hivyo kuikwamua jamii kiuchumi.

Aidha,amesema kwa sasa zipo huduma maalum zinazowalenga kina mama kama akaunti ya Tabasamu na dirisha maalum kwa ajili yao kwenye matawi  ya benki na huduma za bima maisha kwa vikundi ambavyo wanachama wake wengi ni wanawake.

Naye,Mbunge wa Viti Maalum,Fatma Toufiq amewataka wanawake nchini kupendana kuheshimiana pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza huku akiiomba Serikali kuendelea kuwapa kipaumbele katika mambo mbalimbali.

 

Post a Comment

0 Comments