MTAKA AFUNGUA FURSA ZA LISHE KWA WAKULIMA NA WAFANYABIASHARA DODOMA

 


📌JOSEPHINE MTWEVE  NA  AGNESS PETER (DOMECO)

MKUU wa mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amewataka wadau mbalimbali wa lishe kuwekeza katika lishe ili kutokomeza udumavu pamoja na utapiamlo ndani ya mkoa wa Dodoma.

Akizungumza katika warsha ya wadau wa lishe leo jijini Dodoma, Mtaka amesema  ili kutokomeza udumavu pamoja na utapiamlo ni vyema wadau wakawekeza nguvu katika afua za lishe.

Mtaka amesema uwekezaji katika lishe pia unaweza kusaidia ukuaji wa biashara za mazao na kukuza kilimo  cha mazao ya nafaka ikiwemo mtama, soya, mbaazi na maziwa ambayo baadhi uagizwa kutoka mikoa mbaliimbali nje ya mkoa wa Dodoma.

Hakuna haja ya kusafirisha nafaka kutoka nje ya mkoa wa Dodoma wakati tuna uwezo wa kulima hapahapa,kwasababu tuna ardhi nzuri na yenye rutuba katika sehemu tofautitofauti za jiji letu.

Katika kuhakikisha kuwa lishe inakuwa ajenda miongoni mwa wakazi wa mkoa wa Dodoma, Mtaka amesaini mkataba  wa lishe na wakuu wa wilaya 7 za mkoa wa huo ili wakuu hao kuhakikisha wanaenda kupambana na udumazi na utapiamlo katika maeneo yao..

Pia Mtaka amesema wakuu wa wilaya wana kazi ya kuhakikisha nafaka zote zinazohitajika katika lishe zinapatikana katika wilaya zao ili kuongeza upatikanaji wa vyakula vyenye virutubisho ili kuepuka ongezeko la udumavu.

Kuhusu warsha hiyo ya Lishe,Mtaka amesema lengo kuu la kuzungumza na wadau wa lishe ni kuhakikisha wanapata uelewa juu ya lishe ndani ya mkoa na kuelewa kwamba wapo watoto wengi katika jamii waliopata udumavu  kutokana na kukosa  lishe bora hata kwa mama mjamzito na wakati mwingine kupata madhara ukubwani .

Warsha hii ya wadau wa lishe endelevu yaani sustainable nutrition ni kwa lengo la kupata watu wa kujitolea kuboresha lishe endelevu lakini hata kwa watu wengine ambao mmeshiriki katika warsha hii ya leo pia mna jukumu la kushiriki kuboresha lishe.

Aidha  katibu tawala mkoa wa Dodoma, Dk.Fatma Mganga amewataka wadau wa lishe kufanya vizuri zaidi katika kutoa takwimu ya ongezeko la uboreshaji wa lishe endelevu kwa mkoa wa Dodoma na kutokomeza udumavu, ukondefu tofauti na ilivokuwa kwa mwaka huu.

Amesema lengo ni kuimarisha uratibu wa sekta na kuimarisha afya, lishe, maji salama na malezi mazuri kwa watoto kwa kuhakikisha wanapata lishe bora kuanzia majumbani hadi mashuleni katika wilaya zote za mkoa huo.

Tuliahidi kule Kahama, kwamba mwaka ujao tutafanya vizuri kuhusu suala la lishe endelevu kwa mkoa wa Dodoma na naamini tutapata commitment kwa wadau ili kuwezesha fursa ya lishe bora kwa watoto na kuepukana na matatizo lishe mbovu

Moja kati ya shuhuda wa lishe Kelvin Msolwa amesema ameweza kufungua kiwanda ambacho kinazalisha unga lishe wa aina tofautitofauti ikiwemo unga uji wenye lishe pamoja na unga wa ugali wenye lishe.

Msolwa amesema kiwanda chake kina uhitaji mkubwa wa nafaka hasa mtama na uzalishaji wa mtama kwa mkoa wa Dodoma ni asilimia ndogo sana hivyo analazimika kuagiza  nje ya mkoa.

Licha ya kuwa Dodoma kuna uhaba wa mtama lakini nimeweza kuwapa fursa baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma waweze kulima mtama pia nimewakopesha mbegu ambazo zitapandwa kwaajili ya kuzalisha mtama.

Kelvin Msolwa.

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments