UNYANYAPAA KIKWAZO VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA



📌GIMU GALAFONI

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge,Vijana  na wenye ulemavu Jenista Mhagama  amesema licha ya Serikali na Wadau mbalimbali   kuwekeza nguvu kubwa kupambana na matumizi ya Dawa  za kulevya   suala la unyanyapaa kwa vijana  wanaotumia dawa hizo linaonesha kudhorotesha  juhudi hizo na  kufanya matumizi ya Dawa kutokwisha.

Waziri Mhagama amesema hayo  wakati akifungua kikao cha kamati ya bunge ya kudumu ya masuala ya ukimwi na Asasi za kiraia zinazoshirikiana na mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya  jijini Dodoma.

Amesema  jamii imekuwa inawanyanyapaaa watu wanaotoka kwenye Janga la Dawa za kulevya licha ya kuwa wameacha kutumia Dawa hizo hali hiyo inawapelekea watu hao kurejea kwenye matumizi  ya Dawa kutokana na kukosa  upendo na ushirikiano kwa jamii inayowazunguka  hivyo ni vyema kuendelea kuelimisha jamii .

Aidha  waziri Mhagama amesema  asilimia  kubwa ya watumiaji wa dawa hizo ni vijana ambao ni asilimia 56 ya nguvu kazi ya Tanzania  hivyo ni vyema mamlaka  inayohusika na usimamizi wa dawa hizo kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na wabunge ilikuwasaidia vijana hao huku akibainisha juhudi kubwa zilizofanywa na mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) . Patrobas Katambi    amesema  pana uhitaji mkubwa   wa kupata maarifa pamoja  kuongeza tafiti zaidi  huku  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu  Ummy Nderiananga akiahidi kushikiriana na  wadau wa mapambano dawa za kulevya.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Fatma Taufiq amesema wao kama kamati watajitahidi kuhakikisha bajeti inaongezwa katika kupambana na dawa za kulevya huku kamishna wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana dawa za kulevya (DCEA)Gerald Kusaya amesema wamekuwa wakiwawezesha kiuchumi watu walioathirika na dawa za kulevya.

Msimamizi huduma za Afya kwa waraibu dawa  za kulevya kutoka mkoani Arusha Jesca Temu amesema wamekuwa wakifanya juhudi mbalimbali kuwarejesha waraibu katika hali ya kawaida .

Nae Daktari Bingwa wa Magonjwa afya ya akili   na Mwanzilishi wa Huduma za  MAT  hospitali ya Muhimbili Frank Masao  amesema asilimia 83.4 ya watu waliokuwa wanajidunga walikuwa  na matatizo ya ini ambapo Mbunge wa viti Maalum Dkt.Alice Kaijage akihimiza zaidi kuongeza mfuko wa kutosha kwa mamlaka ya kudhibiti dawa  za kulevya

Post a Comment

0 Comments