WAZIRI GWAJIMA AWAPONGEZA WATAALAM WA EPIDEMIOLOJIA NA MAABARA

 



 ðŸ“ŒAGNESS PETER,DOMECO

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt.Dorothy Gwajima, amekipongeza Chama Cha Wataalamu wa Epidemioljia na Maabara  kwa kuanzisha siku ya maadhimisho ya wataalamu wa epidemiolojia na maabara duniani.

Akizungumza na wawakilishi, wananchi na waandishi wa habari leo jijini dodoma, Gwajima amesema anafahamu kwamba ni mara ya kwanza nchini kuadhimisha siku ya wanaepidemiolojia na maabara ambayo kimsingi ni wadadisi wa magonjwa ya kuambukizwa na ambayo sio ya kuambukizwa (Diseases Detective)

Amesema anaamini Shirika la Afya Duniani (WHO) litakubali na kuweka muongozo katika kalenda za shirika lake kwamba siku ya tarehe 07 Septemba itakuwa siku ya maadhimisho hayo na watasubiri muongozo huo .

Ujumbe wa maadhimisho haya kwa mwaka huu ni kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa matukio ya kiafya ili kubaini  haraka matishio ya kiafya katika jamii.

‘’  Nawapongeza wataalamu wote wa epidemiolojia na maabara hapa nchini ambao wengi wao ni wahitimu wa programu ya wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto inayoratibu mafunzo ya kiepidemiolojia na udhibiti wa magonjwa hapa nchini  kwa kushirikiana na chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi Muhimbili,’’amesema.

Amesema utekelezaji wa programu hiyo nchini ni jukumu la Wizara ya Afya kwa kushirikiana na chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi(MUAS) lengo ni kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa afya ya jamii kwa kuboresha uwezo wa kupunguza upungufu wa wataalamu wa kiepidemiolojia na udhibiti wa magonjwa ya chini.

Dkt.Gwajima amesema mafunzo yanatolewa kwa muda wa miezi mitatu au muda wa kati miezi sita kwa kupata cheti au  kukaa miaka miwili na kupata shahada ya uzamifu wa masuala ya sayansi na epidemiolojia, udhibiti wa magonjwa  na masuala ya maabara.



Amesema mafunzo hayo yanatarajia kutoa wataalamu wa epidemiolojia  na sio tu katika afya ya binadamu bali pia katika afya ya wanyama na wataalamu hao watakua na ujuzi wa afya na ufanisi katika ngazi ya jamii na kuweza kutambua magonjwa ya milipuko na matukio mengine yenye hatari za kiafya kwa haraka  na kutoa taarifa katika ngazi ya jamii na wizarani ili yaweze kudhibitiwa kwa wakati.

‘’Wengi watajiuliza hapa kwanini kuna uhusino wa kujifunza kozi hii kwa wanyama na binadamu, ndiyo kwasababu sisi tunaishi na wanyama na wanaweza kutengeneza magonjwa alafu sisi kama hatuna wataalamu hawa wa kuweza kupima nyama inayoenda sokoni tunaweza kukuta tumebeba magonjwa ya wanyama tukaanza kuugua." amebainisha Waziri Gwajima.

Pia Waziri huyo amesema matumizi ya takwimu zenye ubora katika ngazi za chini ili kuweza kufanya maamuzi yenye ushahidi  wa sayansi bado ni changamoto katika halmashauri.


Post a Comment

0 Comments