ASASI ZA KIRAIA ZATAKIWA KUTORUHUSU MIGONGANO NA MIGOGORO


 

Na Saida Issa,Dodoma

Asasi za kiraia nchini zatakiwa kutoruhusu migongano na migogoro Ili ziweze kuzingatia kufanya kazi kwa weledi.

Ili kulinda maslahi na mustakabali wa Taifa ni muhimu kufanya kazi kwa weledi.

Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai ameyasema hayo katika maadhimisho ya wiki ya asasi za kiraia Azaki  yanayofanyika Jijini Dodoma ambapo amesema ni wakati wa asasi hizo kijitathimini na kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria zinazowaongoza.

Aidha amesema mbali na asasi za kiraia kutoa mchango mkubwa katika kujenga nchi lakini Endapo wataruhusu migogoro na migongano ndani ya asasi zao  itakuwa ni jambo Gumu kwao kufanikisha malengo au hazma walizo jiwekea.

Jenipher Kato ni muakilishi wa asasi ya Wote sawa inayojishughulisha na Utoaji Elimu na kutetea wafanyakazi wa majumbani amesema kuwa katika wiki ya asasi za kiraia wanatumia kuelimisha jamii kuhusu wafanyakazi wa majumbani ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa kuwapa wafanyakazi wa ndani mikataba.

Wiki ya asasi za kiraia inafanyika Jijini Dodoma ambapo asasi mbalimbali zinapata nafasi ya kukutana na kujadili mambo yahusuyo asasi hizo pamoja na kutoa Elimu mbalimbali kwa jamii.Post a Comment

0 Comments