Na Zainabu Mtoi, Agness Peter na Josephine Mtweve,

MMILIKI  wa Gazeti la Rai,Jenerali Ulimwengu ameelezea maudhui ya kitabu chake Cha Rai ya Ulimwengu ambayo yanahusu Demokrasia, Utawala wa Sheria na Ukuu wa katiba Tanzania kwa lengo la kushawishi watanzania kuwa na nguvu ya kuzuia uongozi ambao haufuati katiba.

Akizungumza Octoba 06 jijini Dodoma katika mdahalo wa uchambuzi wa kitabu hicho Jenerali Ulimwengu amesema hakuna mahala ambapo Rais amezuia watu kuzungumzia suala la katiba 

"Sijasikia mahala ambapo Rais wetu amesema hataki kusikia mtu akizungumzia suala la katiba na ninapokuwa kwenye vijiwe mbalimbali bado ninasikia watu wanazungumza kuhusu katiba,"amesema.

Ulimwengu ameongeza kuwa ili mtu aweze kugombea hata ukuu wa Kijiji ni lazima awepo katika chama cha siasa kiasi kwamba hawezi kuwa mwanakijiji kamili kwa kugombea hadi ajifiche ndani ya chama fulani cha siasa.

Kwa upande wake Prof.Mussa Assad amesema katiba ya Tanzania ni nzuri na inahitaji kiongozi makini ambapo pia wananchi wanatakiwa kupata nguvu ya kuwawajibisha watawala.

Prof.Assad ameongeza kuwa katiba mpya haiwezi kuwapa suluhisho wananchi bali wanatakiwa kwanza kuwa jamii yenye msingi imara


Post a Comment

0 Comments