SHEIKH MKUU WA DODOMA AWATAKA WAISLAM KUWA KITU KIMOJA.

 

         

Na Zainabu Mtoi, Agness Peter na Josephine Mtweve,

SHEIKH Mkuu wa Dodoma Alhaj Dr.Mustafa Rajabu Shabani amewata waumini wa dini ya kiislam Nchini kuwa kitu kimoja na kuondoa tofauti zilizopo.

Akizungumza katika sherehe za Maulid ya Mazazi ya Mtume Muhammad SAW jana Octoba 25,2021 Kigogo Dar es Salaam mbele ya maelfu ya Waumini kutoka Mikoa mbalimbali Nchini, Sheik Rajabu amesema kuna haja kubwa ya waislam kuungana bila kujali madhehebu.

Amesema kumekuwa na sintofahamu kwa waislam kutofautiana wao kwa wao pasipokua na sababu yoyote ile na kusema ni wakati wa kuondoa tofauti hizo na kuungana kama alivyoelekeza Mtume wa mwenyezi mungu Mtume Muhammad SAW.

"Kuna haja ya waislam Nchini kuungana na kuwa kitu kimoja maana hakuna sababu ya kugombana kisa itikadi zetu wakati dini yetu ni moja.

"Hatuwezi kuendeleza uislam wetu bila kuondoa sintofahamu za hapa na pale2 hivyo tuungane kwa pamoja kama alivyoelekeza Mtume Muhammad SAW kwamba muislam ndugu yake muislam,"alisema.

Sheik Mustafa Rajabu aliambatana na baadhi ya masheik wa wilaya kutoka mkoa wa Dodoma ambao ni pamoja na Sheik wa wilaya ya Kondoa, Sheik wa wilaya ya Chemba, mwakilishi wa Dodoma Jiji Sheikh Abdurahman Issa Mjumbe wa Baraza la Masheik Wilaya ya Dodoma bila kusahau Mjumbe wa Halmashauri Mkoa wa Dodoma.

Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Arusha Sheikh Shabani Juma akizungumza kwa niaba ya Mhe.Muft na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaj Sheikh Abubakar Zuber bin Ally, amesema anawapongeza waislam na watanzania wote kwa ujumla kwa kuendelea kudumisha amani, upendo na mshikamano Nchini na kuwataka Waislam kuendelea kushikamana kwa kufuata misingi ya Dini ya Mwenyezi Mungu.

Maulid ya mazazi ya Mtume Muhammad SAW iliandaliwa na taasisi ya Imamu Swadiq Islamic Foundation chini ya Uongozi wa Sheikh Hemed Jalala.

Katika maulid hayo viongozi na Masheikh wa Wilaya na Mikoa Nchini walibahatika kufika ikiwemo sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Arusha, Morogoro, Manyara na viongozi mbalimbali kutoka Jiji la Dar es salaam bila kusahau Waumini kutoka Tanzania Bara na Visiwani. 


Post a Comment

0 Comments