SHERIA YA BIMA KWA WOTE MBIONI,YASUBIRI BARAKA ZA BUNGE



📌ZENA MOHAMED

SERIKALI imesema ipo mbioni kumaliza changamoto za BIMA binafsi zote za matibabu nchini na kwamba kwa kuanza itajumuishwa wakati wa kujadili sheria  ya huduma ya Bima ya Afya kwa wote ambayo itajadiliwa na Bunge la Novemba  mwaka huu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Dk Dorothy Gwajima  amesema hayo Jijini hapa wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) huku akisema Serikali imejipanga kuhakikisha kila Mtanzania anapata matibabu kwa urahisi, kupitia sheria ya huduma za bima ya afya  kwa wote  na Sheria hiyo itajadiliwa na wabunge Ili ipate maoni na ridhaa kuelekea kuwa sheria.

Serikaki inatambua changamoto zilizopo kwenye mifuko ya bima binafsi,sheria itajadiliwa kuna mifuko ya Bima ya Afya ikiwemo Mifuko wa NHIF, Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Bima zote binafsi zitatazamwa kwenye sheria, wote watajumuishwa na kutazamwa Ili kuwe na tija kwa watoa huduma wote

 Aidha ametaka kuimarishwa kwa udhibiti kwenye eneo la udanganyifu na kuchukua hatua kwa watakaobainika na kusema kuwa tayari Wizara yake imeanza kulifuatilia kwa uzito mkubwa suala Hilo.

 "Tumegundua wafamasia wengi wadanganyifu, wajiandae kujirudisha na wale wanataaluma wajiandae kujibu kwenye bodi na wakirudisha  fedha tutakutathimini kama unafaaa kuwepo kwenye taaaluma au laa,"amesema.

Pamoja na hayo Waziri Gwajima ameeleza kuwa Ili Wananchi wapate huduma bora za bima ya Afya lazima wanataaluma  kuheshimu kazi na kuacha vitendo vya ubadhilifu na kwamba hakuna Kituo kitakachofungwa ila watakaofanya ubadhilifu watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Sambamba na hayo ametaka Mfuko wa NHif nchini  kuweka utaratibu mzuri  wa kujisajili hasa maeneo ya Vijijini ili wanachama waweze kujisajili na kuondokana na usumbufu uliopo kwa Sasa.

Kutokana na hayo,aliyewahi kuwa Waziri wa Afya wakati Mfuko huo unaanzishwa mwaka 2001,Anna Abdallah amesema utashi wa kisasa ulichangia kwa kiasi kikubwa kukua Kwa mfúko wa NHIF.

 Amesema licha ya ugumu uliokuwepo wa  ushawishi kwa jamii kuhusu mfúko huo Bado walisimama kwenye nguzo moja ambàyo ndiyo iliwapa matumaini ya kutokata tamaa na kusababisha mafanikio yaliyopo Sasa.

Ameeleza kuwa mafanikio ya Sasa yametokana na kuzikabili changamoto za mfúko huo na kuwa fursa 

Watanzania wengi wanapenda kutumia Bima ya Afya hata sasa ukifika Hospitali unaulizwa kama una kadi ya Bima ni jambo la kujivunia  sana,wakati tunaanza jambo hili wengi walidharau,ikifika wakati hata wale Wenye bima walienda Hospitali kutibiwa walinyanyapaliwa ,Sasa wanaheshimika

 Alisema japo safari mwanzoni ilikuwa ngumu lakini Mfuko unaendelea kufanya vizuri na kuwa njia za kisasa," alisema.

Mwenyekiti wa Bodi Mstaafu, Anna Makinda alisema, walipokuwa walianza walijibunia wataalam wa Bima lakini.baafae waliambiwa mfumo hauzungumzo na sasa kuna Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) 

"Tunapokwenda ni kwema kwani leo mtu kama hana kadi ya Bima anajilaumu," alisema.

Mmoja wa Wajumbe wa bodi,Magreth Sitta amesema awali walimu walipinga ila ilisaidia zaidi kuboresha mfumo

Walikuwa na wasiwasi je Kijijini walipo watapata huduma lakini msimamo wao ulisaidia na sasa kuna vituo vya afya na zahanati zinajengwa Vijijini

Ametumia nafasi hiyo kuitaka Serikali itoe elimu watu waelewe  zaidi watakavyonufaika na mfuko huo Kwani wengine Hadi Sasa hawaelewi na kujikuta  wanaenda kukata Bima wakati wakiwa na wagonjwa nyumbani  wakati kadi inapatikana baada ya mwezi moja.

 Kwa maboresho zaidi ameshauri Serikali Kupitia Wizara ya afya  iangalie namna ya kuhudumia Wazee hasa wa Vijijini kama dawa hakuna alipo ni mbali na mjini wanakosa matibabu na wengi Wana changamoto ya umri.

 Mwenyekiti wa kwanza wa Bodi ya NHIF, Profesa Lucian Msambichaka alisema changamoto kubwa ilikuwa ni uelewa hasa kwenye suala la hisa huku akimtupia lawama Dk Gwajima kuwa alikuwa kikwazo wakati mfuko huo ulipoanza wakati huo akiwa Mganga Mkuu wa Singida.

 "Mh.Waziri sikuteti,hata wewe ulitupa wakati mgumu wakati tunaaza,nashukuru baadaye ulituelewa na kukubali kutupa ushirikiano, wakati akiwa Mganga Mkuu Singida ulisaidia sana kutangaza Mfuko na Mkoa wa Singida ulifanya vizuri na kuwa mfano,' amesema

Amesema ,wananchi wengi hawakuwa na uelewa wa dhana nzima ya bima huku wengi wao wakiamini Kuwa na Bima ya afya mkononi ni sawa na kujitabiria magonjwa .

 Walipoambiwa walipie asilimia kadhaa waliona kama ni dhuluma lakini kama bodi hilo halikutushangaza,tuliona kama jambo la kawaida,Walimu ndio walikuwa wagumu na tulichukulia kama changamoto,"amesisitiza.

 Prof.Msambichaka amesema Mfuko ulikuwa mchanga lakini Rais wa awamu ya tatu Hayati Benjamin Mkapa alisimama na Mfuko ukaanza kutekekeza majukumu yake bila kuyumba.

Wengi walikuwa hawaamini kama tutakwenda wenyewe bila utaalam kutoka nje, lakini  marehemu Mkapa alisimama na kuwezesha zaidi  msaada wa fedha na kusaidia kuondosha changamoto ikiwemo Hospitali kupokea wagonjwa wenye bima na kuwapa kipaumbeli

 Hata hivyo amependekeza bodi na menejimenti ya NHIF wakamilishe mkakati endelevu kuelimisha wananchi juu ya Bima ya Afya ili wananchi wengi zaidi wajiunge na Mfuko huo na kuwekeza zaidi kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

 Naye Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya huduma za Jamii Silvester Nyongo amesema wao Kama wadau wa afya nchini  wataendelea kuwa tayari kutoa ushirikiano na kuhakikisha wanafanikisha yale yote waliyopangwa.

 Kuna changamoto nyingi bado ziko kwenye Mfuko wa NHIF lakini changamoto zake zinapelekwa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF, jambo hili linatakiwa kuangaliwa,mzigo wa mfuko mwingine haupaswi kuhamishiwa kwenye mfuko mwingine

Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa NHIF, Emmanuel Humba alisema Mfuko umepitia changamoto nyingi wakati unaanzishwa lakini sasa wanajivunia mafanikio ya Mfuko na huduma nzuri zinatolewa na Mfuko.

Kutokana na hayo ametaka kuendelea kutolewa kwa elimu zaidi ya Bima ya afya na kuwezesha watanzania wengi zaidi wafaidike.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Benard Konga amesema  kuna vituo vya afya  14,000 Nchini ambavyo mfumo wa TEHAMA unafanya kazi hivyo kuwataka wateja wake  kuwasilisha madai na malalamiko yao Kwa kutumia njia ya TEHAMA.

Mkurugenzi huyo amesema Kwa sasa wanahudumia wanachama milioni 4.5 na wataendelea kuwekeza kwenye TEHAMA  Ili waweze kuhudumia wananchi wengi zaidi.

 

Post a Comment

0 Comments