''TANZANIA HUTUMIA ASILIMIA 2 HADI 3 YA PATO LA TAIFSA KUKABILIANA NA MADHARA YA TABIANCHI''-WAZIRI HAFO



 Na Rhoda  Simba,Dodoma.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Seleman Jafo amesema nchi ya Tanzania hutumia asilimia 2 mpaka 3 ya pato la taifa katika kukabiliana na madhara ya tabianchi. 

Waziri Jafo ameyasema hayo Octoba 1 jijini Dodoma mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu msimamo wa Tanzania kwenye majadiliano  ya mkutano  wa 26 wa Nchi  wanachama wa Mkataba wa umoja wa mataifa Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi 

Waziri Jafo amesema  fedha hizo ni nyingi ukizingatia hali ya uchumi wa Tanzania na vipaumbele vya Serikali katika kuleta maendeleo kwa watu wake. 

Amesema mkutano huo unafanyika katika kipindi ambacho shirika la umoja wa Mataifa la hali ya hewa Duniani limetoa taarifa inayothibitisha kuwepo kwa ongezeko la joto katika uso wa dunia ambapo kuongezeka kwa kiwango cha joto kumesababisha athari za mabadiliko ya Tabia nchi katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.

"Athari hizo ni pamoja na kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari kuliko sababisha kisiwa cha maziwa Wilaya ya Pangani na kisiwa cha fungu la Nyani Wilaya ya Rufiji kumezwa na maji ya bahari,"

"Katika msimu wa mwaka 2019 mpaka 2020 mvua zilisababisha kuongezeka kwa kina cha maji kwenye ziwa Victoria na ziwa Tanganyika huku miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mafuriko ya mara kwa mara na ukame wa muda mrefu kwenye baadhi ya maeneo nchini," amesema Waziri Jafo.

Amesema pamoja na ukweli kwamba Tanzania sio miongoni mwa nchi zinazozalisha gesi joto kwa wingi duniani serikali  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imechukua hatua za kukabiliana na athari zamabadiko ya Tabianchi zikiwemo kujenga uwezo wa kitaasisi kutoa elimu kwa jamii na kuhimiza shughuli za kilimo,Ufugaji na Uvuvi zinazostahimili mabadiliko ya tabianchi .

Katika mkutano huo Tanzania itashirikiana kikamilifu katikamajadiliano ya masuala yenye maslahi mapana kwa nchi yetu na kuweka misimamo wake kwa yafatayo Rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mkataba na makubaliano ya Paris, kujenga uwezo, Kilimo na mabadiliko ya tabianchi ,Uendelezaji na usambazaji wa Teknolojia,Mchango wa taifa wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi,Upunguzaji gesjoto kwa kutumia biashara na Jinsia na mabadiliko ya Tabianchi. 

Hata hivyo mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba huo utafanyika jijini Glasgrow nchini Scotland kuanzia octoba 31 mpaka novemba 12 mwaka 2021 na utahudhuriwa na wajumbe 3000 kutoka nchi mbalimbali duniani wakiwemo wakuu wa nchi na serikali ,mawaziri na wataalam waliobobea katika maswala ya tabia ya nchi.


Post a Comment

0 Comments