KAMISHNA SABAS KUFUNGA MAFUNZO YA MEDANI ZA KIVITA KWA WANAFUNZI WA KOZI YA UOFISA

 


Kamishna wa Operasheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi (CP) Liberatus Sabas anatarajiwa kufunga mafunzo ya medani za kivita kwa maafisa wa jeshi hilo katika kambi ya Mkomazi mkoani Tanga.

Kamishana Sabas atafunga kozi hiyo hapo kesho (27/11/2021) ikiwa ni wiki ya mbili tangu kuanza kwa mafunzo hayo yaliyojumuisha maafisa wa Polisi 749 kuanzia tarehe 13/11/2021.

Mafunzo hayo yanaendeshwa na chuo cha taaluma ya Polisi cha Dar Salaam(DSM Police Academy) na  yalianza rasmi tarehe 18 June katika hatua za awali kabla ya kuhamia Mkomazi kwa mafunzo ya medani.


Mkuu wa Chuo cha Taalum ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akiongea na wanafunzi wa kozi ya Uofisa baada ya kukagua maandalizi ya sherehe za kufunga mafunzo hayo katika Kambi ya mafunzo ya medani za kivita Mkomazi mkoani Tanga.

Aliyesimama nyuma ni Mkufunzi mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, ACP Lutusyo Mwakyusa. Mafunzo hayo yanatarajiwa kufungwa kesho




Mkuu wa chuo akiwatunukia zawadi ya fedha wanafunzi wa kike waliofanya vizuri kwenye mazoezi ya maandalizi ya kufunga mafunzo 

 


Post a Comment

0 Comments