NAIBU SPIKA WA BUNGE DK.TULIA AWAPA NENO ATCL

  


Na Saida Issa, Dodoma


Naibu Spika Dk.Tulia Ackson amelitaka Shirika la ndege Tanzania (ATCL) kuhakikisha linajiendesha kwa tija na kwa faida ili kuondoa dhana mbaya  iliyojengeka kwa baadhi  ya watu kuona linajiendesha kwa hasara.

Dk. Tulia ameyasema hayo mara baada yakukutana na kamati mbalimbali za Bunge na shirikia hilo ambapo amesema changamoto zinazosemwa kama zikifanyiwa kazi ni wazi zitaleta mabadiliko chanya kwa wananchi.

"Mashirika yetu haya kama yatasimamiwa vizuri yatakuwa na tija na yataleta mafanikio chanya kwa Taifa letu,pia sisi kama bunge tutakuwa karibu na Shirika letu hili Ili kuweza kuona kwa ukaribu changamoto zinazoikabili Shirika letu,"amesema  Tulia.

Aidha alisema wabunge kama wawakilishi wa wananchi walipata uelewa juu ya shirika la ndege la Taifa litawapa uelewa kwani wakielewa wao wanachi pia wataelewa kwani watakuwa mabalozi Wazuri kwa kulisemea Shirika.

"Tukipata uelewa sie ni rahisi sana kuwa mabalozi hasa kwa kuwaelimisha wananchi wetu na wao waweze kuwa na uelewa juu ya shirika letu hili la ndege,"ameeleza Naibu Spika.


Post a Comment

0 Comments