📌HAMIDA RAMADHAN
TAASISI za Serikali zimetakiwa kununua Mifumo au miundombinu ya tehama iliyo Salama na inayoendana na malengo ya Taasisi zao na zimetakiwa zifanye Uchambuzi wa kina na zianishe mahitaji ili waweze kununua mfumo husika .
Akiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi za mamlaka mtandao katika mji wa serikali Mtumba wakati akihitimisha wiki ya ya uelimishaji umma kuhusu Sheria ya serikali mtandao Jijini hapa kamishina Msaidizi wa Jeshi la polisi na Meneja wa huduma za Sheria- Mamlaka ya Serikali mtandao (EGA) Raphael Rutaihwa amesema mamlaka hiyo lazima isimamimie Taasisi za serikali kununua Mifumo ya tehama inayoendana na mahitaji yao na itakayoweza kutatua matatizo ya Mifumo.
Lazima tuangalie matataizo gani kwenye Taasisi zetu na tunataka kupata tija gani,na tunataka kuwekeza kiasi gani kwa sababu Mifumo ni uwekezaji mkubwa na inachukua kiwango kikubwa cha pesa lazima tujue thamani ya fedha bila kusahau tija kwani tu atakuwa kufahamu tumepata tija gani kulingana na uwekezaji wetu kwenye Mifumo
Aidha amesema mamlaka imepewa jukumu la kuhakikisha kwamba inawezesha Taasisi za umma Mifumo iliyojengwa inakuwa Salama na ndio maana imekuwa ikifanya tathimini ya mara kwa mara kwa kushirikiana na vyombo vingine ili kuhakikisha Mifumo inayotumika serikali ni inakuwa Salama kwa maana taarifa za serikali haiwezekani kuvuja
Amesema Usalama la Mifumo ni jukumu la mamlaka kwa kushirikiana na Taasisi za umma na hiyo imekuwa ikifanyika kwa kuwawezesha wataalamu waliopo katika taasisisi za umma au kuzishauri taasisi za umma kuwa uwezo wa mara kwa mara kwani teknolojia imekuwa ikibadilika kila siku.
Pia Sheria namba 10 ya wala 2019O ya serikali mtandao inaelekeza Taasisi yoyote ya umma isijenge wala kuendeleza Mradi wowote wa tehama bila kupata Idhini ya mamlaka.
Sheria
imeelekeza Taasisi zote za umma chini ya mamlaka zifanye tafiti ya Mifumo
itakayoweza kusaidia matatizo ya nchi.
0 Comments