📌RHODA SIMBA
SHIRIKA la viwango Tanzania TBS kwa kushirikiana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo SIDO, wameanza kutoa elimu kwa wakulima na wazalishaji pamoja na wasindikaji wadogo wadogo wa zao la zabibu lengo likiwa ni kuhakikisha wanazalisha wine bora na yenye viwango ili kuweza kushindana na bidhaa zinazozalishwa nje ya Nchi.
Hayo yamesemwa leo Novemba 15 jijini hapa wakati akifungua semina ya wajasiriamali katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Dodoma Aziza Mumba ambapo amesema Serikali inatambua mnyororo wa thamani hasa katika zao la zabibu.
Amesema kwa hapa Dodoma zao la Zabibu ni la kimkakati na lengo ni wakulima wauze huku Serikali na wawekezaji wakiangalia namna ya kuanzisha viwanda zaidi vya kusindika zabibu ziwe juice na kwamba tayari Kuna viwanda vidogo 18 na vya Kati 3.
"Nashukuru TBS kwa kufanya haya mafunzo kuwapatia ujuzi na kuwajengea uwezo ili wawe jasiri Katika usindikaji wa zabibu jambo ambalo litawasaidia sana Katika kuongeza kipato chao na kupata soko kubwa ndani na nje ya nchi "Amesema Mumba
Nae Meneja wa Shirika la Viwango
Tanzania (TBS) Kanda ya Kati ,Nickonia Mwabuka Amesema kuwa
TBS imeandaa mafunzo haya kwa kushirikiana na sido lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora na usalama hatimaye kujikwamua kiuchumi.
"TBS inasaidia kupima bidhaa
hizi ili ziweze kuwa na soko za Kimataifa na mpaka Sasa Wasindikaji 15
wamefaidikia na mfumo huu na kupitia mafunzo haya yatafanikiwa kwa Kiasi
kikubwa "Amesema Mwabuka
0 Comments