UZUSHI : REAL MADRID HAIJAMPONGEZA KOCHA MPYA WA SIMBA

 


📌RHODA SIMBA, DODOMA
.

NI Majumaa kadhaa yamepita tangu wekundu wa msimbazi  Simba waachane  na aliyekuwa   kocha wa  klabu hiyo Didier Gomez da Rosa ambae alihudumu kwa msimu  mmoja tu.

Mara baada ya kufanya vibaya kwenye michuano ya kimataifa na nafasi yake kukaimiwa na kocha msaidizi Thiery Hitimana kwa  kushirikiana na  Suleiman Matola mpaka pale Simba walipomtangaza  Pablo Franco Martini kama kocha mkuu.

Mara baada  ya Simba kumtangaza  Pablo kuwa kocha mkuu wa Klabu hiyo kumekuwa na maneno yanayosemwa  kuhusiana na maisha yake ya soka hususani timu ambazo amewahi kuzifundisha ikiwemo Real Madrid ambapo alikuwa kocha msaidizi chini ya  mfaransa Zinadine Zidane   mwaka 2018/2019.

Kuna picha inayo onesha kuwa ni ukurusa rasmi wa Twitter ya  Real madrid C.F. ikionesha  timu ya hiyo imempongeza Pablo Franco Martín   kwa kujiunga na  Simba  katika tasfri isiyo rasmi ya kiswahili inasema “Klabu inatoa shukrani zake za dhati kwa kocha wetu msaidizi @ pablofrancomartin kwa kufanya kazi nasi kama kocha msaidizi.Tunatakutakia mafanikio mema kwenye Klabu yake mpya ya Simba Asante Pablo




Ukweli ukoje

Ukweli ni kwamba habari hiyo siyo ya kweli.Kwanza ukurasa uliotoa habari hiyo  siyo ukurasa  rasmi wa twitter wa  timu ya Real Madrid bali ni moja  kati ya  ukurasa za mitandaoni zinazotumika kutoa  taarifa za uzushi.


Central Press Club  imefanya tafiti kwenye kurasa rasmi zote  tatu Twitter ya Real Madrid @realmadrid ambazo zipo katika lugha ya kiingereza, kifaransa na kihispaniola na kugundua kuwa hakuna salamu za namna hiyo na ni uzushi mtupu unao sambazwa.

Jambo lingine linalotia shaka katika Twitter hiyo  ya uongo ya real madrid ambayo imenukuu Twitter ya uongo ya kocha mpya wa Simba kwa kuandika@ pablofrancomartin  wakati ukweli ukurasa rasmi wa kocha huyo mpya wa  simba Pablo Franco Martín ni@FrancoMPablo.

Pia kurusa zote zilizothibitishwa na Twitter ziwe za taasisi ama mtu mmoja mmoja zimekuwa na alama au tiki ya blu lakini hii inayodai ni ukurasa rasmi wa Klabu ya Real Madrid na ambayo inadai umethibitishwa imewekewa alama au tiki nyeupe badala ya blu.

Licha ya Pablo Franko Martini kuwahi kufundisha timu  mbalimbali ikiwemo Real Madrid kama kocha msaidizi, Beijing kama kocha msaidizi ,,Getafe  CF  kocha mkuu, CD PUERTOLANO  kama kocha mkuu,  pamoja na CD  SANTA EUGENIA kama kocha mkuu lakini Real Madrid hawajampongeza ni uzushi mtupu.

 

 

 

Post a Comment

0 Comments