📌RHODA SIMBA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mohamed Mchengerwa amewataka viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufatilia vyema utekelezaji wa miradi yote ya kimaendeleo inayoendelea hapa nchini na wahakikishe kuwa kusiwepo na mianya ya rushwa
Aidha amewaagiza viongozi hao kuongeza jitihada katika kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujua haki zao na waweze kuepukana na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa.
Ameyasema hayo leo
octoba 25 jijini hapa wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi
60 kutoka katika wilaya 28 za kitakukuru, wenye lengo la kujadili utendaji
kazi, pamoja na changamoto katika kazi zao.
“Utekelezaji wa miradi
ya kiimaendeleo umegubikwa na udanganyifu ninyi kama TAKUKURU kiongozi wa
kila wilaya apimwe namna anavyoweza kusimamia matumizi ya fedha katika
kila wilaya na niseme tu kwamba hili ni jukumu letu sotekatika
kusimamia kusimamia,
“Mheshimiwa Rais wetu
Samia Suluhu Hassan alivyofungua hizi fursa za uchumi hakumaanisha watu
watumie fedha hizo vibaya na kutumia nyaraka za uongo kuhusu gharama
zinazotumika katika miradi hiyo tumieni mkutano huu kujadili malengo
na muhakikishe kusiwepo na mianya ya uchepushaji wa fedha hizo kwaajili ya
matumizi binafsi katika kila mradi”amesema Mchengerwa.
Aidha amesema Taasisi
hiyo isionekane na kasoro ya rushwa na badala yake iwe mstari wa ,mbele
kufanya kazi usiku na mchana ili kuokoa rasilimali za taifa .
Naye Mkuu wa Wilaya ya
Kondoa Hamis Mkanachi akiongea kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthon
Mtaka amewataka viongozi hao kutumia mkutano huo kujadili tathimini ya
mwaka mzima na Zaidi wajikite katika kutatua uzembe pamoja na kutowajibika
kwa baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo.
Wito wangu kwenu ni kwamba tathmini yetu iwe ya kina na tutazame namna tutakavyoweza kujipambanua katika kila wilaya namna bora ya utendaji.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mkuu kutoka katika Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
TAKUKURU Salumu Hamduni amesema wametekeleza majukumu na kwa
kipindi cha mwaka 2020 hadi 2021 jumla ya shilingi billion 29.3
ziliokolewa ambapo billion 11 .2 ziliokolewa kwa mfumo wa fedha taslim na
utaifishaji mali na kiasi cha bilioni 18 zilidhibitiwa kabla
hazijatumika.
Amesema miradi ya
kimaendeleo 1,188 zenye thaman ya billion 714.17 katika sekta ya afya
maji elimu ziliweza kufatiliwa na kuona makosa ambayo
wameyachukulia hatua.
Tumeelimisha katika ngazi ya makao makuu pamoja na wakuu wa takukuru kuzuia vitendo vya rushwa kuelimisha, kushirikisha jamii pamoja na kuwafikisha watumiwa mahakami kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya mashtaka majalada 1,053 yalichunguzwa na kukamilishwa .
Pia amesema katka majalada hayo,majadala 339 yaliwasilishwa kwa mkurugenzi wa mashitaka kuomba kibali cha kuwafikisha mahakani ambapo kesi mpya zilipatikana 542, na kesi 541 zilitolewa uamuzi ambapo Jamhuri iliweza kushinda kesi 345.
Aidha akizungumzia
changamoto zinazoikabili Taasisi hiyo Hamduni amesema ni pamoja na ufinyu wa
bajeti ambao umeathiri uchunguzi, mafunzo kwa wafanyakazi, ununuzi wa vifaa na
mahitaji mbalimbali pamoja na uhaba wa wafanyakazi
Hata hivyo Mkutano huo
wa siku tatu wa viongozi wa TAKUKURU umebebwa na kauli mbiu isemayo ”
kupambana na rushwa ni jukumu lako”
0 Comments