WAZIRI UMMY AKERWA NA MASHARTI MGUMU KIDATO CHA KWANZA,ATOA TAMKO

 


📌RHODA SIMBA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewaagiza  Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya na Watendaji wa Halmashauri zote nchini kusimamia kusiwe na vikwazo kwa wanafunzi  pale wanapoenda kujiunga na kidato cha kwanza.

Kadhalika amewataka wakuu wa shule kuzingatia kwamba kuna baadhi ya wanafunzi wanaotoka katika familia duni na pale  wanapoenda kujiunga na shule wasiweke masharti magumu hususani kwenye mahitaji ya kwenda nayo shule ambayo yatawafanya washindwe kujiunga.

Ameyasema hayo leo octoba 24 jijini hapa wakati akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi  wa kidato cha kwanza  kwa mwaka 2022 ambapo jumla ya  wanafunzi 907,802 wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza.

“Tarehe 30 Octoba Baraza la Taifa la mitihani lilitoa matokeo ya waliomaliza darasa la saba ambapo jumla ya wanafunzi  waliofanya mitihani milioni moja 107,460  na kwamba kati ya hao wanafunzi laki 907,802 wamefaulu katika mitihani hiyo,

“Ofisi ya Rais TAMISEMI  kwa kushirikiana na Wizara ya elimu imekamilisha zoezi hilo la  kuwapangia wanafunzi shule kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2022 na zoezi hili limehusisha jumla ya wanafunzi  907,802 kati ya hao wasichana 467,967  wavulana 439,835 sawa na asimilia 81.9 ya wanafunzi waliyofanya mitihani ya kuhitimu” amesema Ummy

Aidha amesema kati ya wanafunzi hao wenye  mahitaji maalumu waliofanikiwa kupangiwa kujiunga na  kidato cha kwanza ni wanafunzi 2673   ni wanafunzi wenye mahitaji maalumu sawa na asilimia 0.29 ya wanafunzi wenye ulemavu ambapo kati ya hao wavulana ni 1471 wasichana 1202.

Tumeangalia wanafunzi waliofaulu mwaka jana kulinganisha na mwaka huu ambapo  tumeona kumekuwa na ongezo la  wanafunzi 73,932 sawa na ongezeko la asilimia 8.87

Akizungumzia  kuhusu mfumo wa uchaguzi amesema  mwaka huu uchaguzi wa wanafunzi umefanyika katika mfumo wa kielectronic ambapo umesaidia mambo kadhaa ikiwemo  kupunguza muda wa uchaguzi, gharama, na upangaji wa wanafunzi na limeondoa upendelo na mfumo umetenda haki kwa kuangalia  ufaulu wa juu.

“Nipende kusema kuwa mfumo umeongeza ufanisi kutokana na wanafunzi kupangwa kama mfumo unavyoelekeza na Serikali imefanya maandalizi mapema ya wanafunzi wote wamechaguliwa kujiunga na shule zetu za sekondari na wataanza siku moja mara muhula utakapoanza  na tunatarajia utaanza tarehe 17 january “

Matarajio yetu kwa jitihada za serikali wanafunzi wote watakuwa darasani kwa siku moja na nichukue nafasi hii kumshukuru Rais  Samia Suluhu Hassan  kwa kutenga kiasi cha shilingi billion 240   katika ujenzi wa madarasa elfu 12 nchi nzima

Hata hivyo mesema Vigezo vilivyotumiwa kwa wanafunzi katika ufaulu ni kupata asilimia 121 hadi 300 kwa alama 300 ambapo kila somo lilikuwa linabeba alama 50 katika kila somo kwa  masomo sita.

 

Post a Comment

0 Comments