RADIO ZA KIJAMII ZATAKIWA KUENZI MAUDHUI YENYE MAADILI



 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

REDIO za kijamii zimetakiwa kuendelea kuandaa maudhui yanayozingatia maadili na miiko ya kitanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo Disemba 7 jijini hapa na Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Emmanuel Buhohela wakati  akifungua kongamano  la redio  za kijamii  lililoandaliwa na mtandao wa redio za  kijamii Tanzania ( TADIO) ,Mtandao  wa Kutoa Huduma za Redio Afrika Mashariki  (EARS) na Shirika la Habari la Kuchochea Mabadiliko la Ujerumani.

Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  inathamini   umuhimu  wa  vyombo vya habari  hasa redio  za kijamii ambazo zinawafikia  watu  wengi hasa   sehemu za vijijini .

Aidha amezitaka redio za kijamii kuendelea kuandaa maudhui yanayozingatia maadili na miiko ya kitanzania.

Amesema  mchango wa redio za kijamii ni mkubwa kwani wananchi wengi wanafikiwa na redio hizo zimekua ni sehemu muhimu  za kusambaza  taarifa na ni ukweli ulio wazi  kwamba   uandishi  wa habari zinazojali  maisha  na kero za watu huchangia kwa kiasi kikubwa kujenga uelewa na  kupunguza umasikini .

TADIO mnafanya  kazi kubwa sana, nimeambiwa mtandao wenu unawafikia asilimia 70 ya Watanzania hasa waliopo vijijini. haya ni mawanda makubwa sana ya kuifikia  jamii kimawasiliano

Amesema  Serikali  inafanya kila juhudi kuimarisha umoja wa wana Afrika  ya Mashariki na uimara wa  Jumuiya ya  watu wa  Afrika Mashariki inategemea   ubadilishanaji  wa  taarifa,uwepo  wa redio hizi  za kijamii  na mahusiano  yatakayo imarisha  umoja huo  na kubadilisha  taarifa , ujuzi  wa   kitaalamu  na hata fursa ambazo zinaweza kuchangia maendeleo .

Amesema kuna changamoto  nyingi zinazozikabili radio za kijamii ikiwemo uwezo mdogo  wa kifedha , uwezo wa kitaaluma miongoni  mwa watendaji changamoto ya tozo na kodi mbalimbali.

“Niwahakishe kwamba serikali inajitahidi sana kuhakikisha kwamba tasnia ya habari inakuwa  hasa maendeleo endelevu  ya redio  za kijamii  . kwa hili naomba tukae pamoja , tutafakari na tupange mipango  ya pamoja ya kuwa na mipango  endelevu ya kuziimarisha redio  zetu na  kuondoa vikwazo,” amesema Buhohela

Nae Kaimu mkurugenzi wa TADIO, Baptist John amesema TADIO ina wanachama 34 na press club moja  ambayo ni ya Pemba.

Hata hivyo amesema uanzishwaji wa redio jamii sio rahisi na changamoto iliyopo ni uendeshaji na namna ya kuwawezesha waandishi kuwa na mapato yanayojitosheleza ili kuwasaidia wasiwe wanapotosha taarifa katika jamii.

Post a Comment

0 Comments