RAIS SAMIA KUITENGAISHA WIZARA YA AFYA NA MAENDELEO YA JAMII

 


📌WAMJW

RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan anakusudia kuitenganisha Wizara ya Afya ili kuunda wizara mbili ili kuboresha ufanisi wa kutoa huduma kwa jamii.

Amebainisha hayo leo Tarehe 16 Desemba 2021 jijini Dodoma katika uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Utekelezaji wa Ahadi za Nchi kuhusu Haki za Kiuchumi kwa Wanawake ambalo ni eneo muhimu katika kufikia Kizazi chenye Usawa ambapo kamati hiyo yenye wajumbe 25 kutoka sekta mbalimbali ambao wanatarajiwa kufanikisha kumuinua mwanamke kiuchumi

Rais Samia amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa nusu ya watu Duniani ni wanawake bado sehemu kubwa ya dunia haijatoa nafasi sitahiki kuitumia ipasavyo nguvu kazi ya wanawake ambao wakitumika vema wanauwezo mkubwa wa kuchangia uchumi wa Dunia dola za kimarekani Tilioni 28 kwa mwaka.

" Maamuzi yangu ni kuitenga wizara itakayo shughulikia Jinsia Maendeleo ya Jamii,Jinsia,,Wazee na Watoto kutoka kwenye kuchanganywa na Wizara ya Afya kwa sababu tukiweka Wizara ya afya na hali tuliyonayo sasa duniani sekta ya Afya peke yake inachukua sura kubwa ya wizara hii kuliko vipengele vingine vilivyobaki lakini kama tutatenga vipengele vingine ili Afya isimame peke yake usimamizi wa sera sheria na mambo mengine unaweza kwenda vizuri kwa msukumo unaohitajika" amesema Mhe.Samia Rais wa Tanzania

Awali akitoa taarifa kwa Mhe.Ras Samia, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima amesema kuwa kutokana maagizo ya mkutano wa June 8 2021 jijini Dodoma Wizara zinazoshughulikia maswala ya Jinsia upande wa Tanzabnia Bara na Zanzibar ilianza kulifanyia kazi agizo kwa kuhakikisha kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatimiza ahadi yake ya kuwa  kinara katika eneo la haki na usawa wa kiuchumi.

Kutokana na usawa huo, wanawake na wanaume watakuwa na fursa na haki sawa katika kunufaika na uwezeshaji kiuchumi. Pamoja na kuzindua Kamati hii leo,  Wizara  pia imeweza kuratibu uandaliwaji wa Mpangokazi Jumuishi na Shirikishi  wa Taifa.

Post a Comment

0 Comments