MATUKIO YA MAUAJI MWEZI JANUARI NI 179,SERIKALI YAUNDA KAMATI MAALUM KUTAFUTA SULUHISHO

📌RHODA SIMBA

SERIKALI imesema vitendo vya kikatili vinavyoendelea nchini ambapo kwa muda wa mwezi mmoja (January 2022)  matukio 179  yamejitokeza huku watuhumiwa zaidi ya 150 wakitiwa mbaroni,vinapaswa kukemewa na vinahitaji ushiriki wa wananchi katika kuvitokomeza.

Kauli hiyo imetolewa  hii leo jijini hapa na Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Yusuph Masauni katika kikao chake  na Uongozi wa juu wa Jeshi la Polisi kujadili matukio ya mauaji yanayoendelea nchini.

Katika hatua ya kupambana na matukio hayo Waziri Masauni ametangaza kuunda kwa kamati ili kupata ufumbuzi wa kudumu kwa kujiridhisha na kufanya tathmini ili kujua nini kifanyike ambapo amepokea taarifa ya mwezi mmoja ya kuhusiana na matukio hayo.

Kamati hiyo imeundwa kwa kuhusisha vyombo vya ulinzi ikiwemo Jeshi la Polisi na idara ya Usalama wa Taifa,TAKUKURU,Ofisi ya Mwendesha mashtaka pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kamati hiyo pia inaundwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Ustawi wa Jamii Pamoja wadau kutoka Elimu ya Juu.

Serikali ya Rais Samia inasikitishwa sana na matukio yanayoendelea sisi kama Jeshi la polisi pamoja na Serikali hatulali tuko macho muda wote kuhakikisha matukio ya kihalifu yanayoendelea yanaishi haraka

Serikali haipendezwi kabisa na hii hali tuko macho na pale tunapobaini tukio limetokea hatua za haraka zinachukuliwa mara moja na kuhakikisha wahusika wanabainika na hapo hapo hatua Kali zinafuatwa,"amesema.

Aidha Waziri Masauni amesema kuwa matukio mengi yamekuwa yakitokana na visa,kulipa kisasi,wivu wa mapenzi,migogoro ya ardhi,ulevi pamoja na ushirikiana hali inayosababisha watu kujichukulia Sheria mkononi.

Matukio yote haya yamekuwa yakitokana na visa tofauti tofauti hii inapelekea watu kujichukulia Sheria mkononi hii niwatoe hofu watanzania Serikali ipo makini na yeyote anayethubutu kufanya uhalifu asidhani kuwa Jeshi la polisi litamfumbia macho kila mtuhumiwa atapata jukumu yake kwa mujibu wa Sheria.

Hata hivyo Masauni amelitaka jeshi la Polisi nchini kuhakikisha watuhumiwa wote wa mauji wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria huku akisema kwamba hakuna mtu ambaye atafanya mauaji katika ardhi ya Tanzania na akatoka salama.

Pia amewataka watanzania kuweza kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi pindi wanaposhuhudia matukio ya ukatili bila kusita kwani watasaidia kumaliza matukio hayo.

 

Post a Comment

0 Comments