SERIKALI KUANZISHA SHERIA KUWATAMBUA MADALALI NA HAKI YA MPANGAJI

 


📌RHODA SIMBA

SERIKALI imesema ipo katika mchakato wa kuanzisha Sheria  ya Mamlaka ya usimamizi wa biashara ya upangaji wa ardhi na majengo itakayotambua na kuainisha haki za wapangaji, haki za madalali na watu wenye sifa ya kufanya biashara hiyo.

Hayo yamesemwa leo Januari 7 jijini hapa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi wakati wa uzinduzi wa kituo cha huduma kwa mteja katika Ofisi za Wizara ya Ardhi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba  lengo likiwa ni kupunguza gharama pamoja na kujikinga na ugonjwa wa uviko 19.

Waziri Lukuvi amesema Mamlaka hiyo itasimamia shughuli zote za biashara ya upangaji na kuondoa kilio cha muda mrefu cha wananchi kuzulumiwa na madalali pamoja na kuiwezesha serikali kukusanya kodi na tozo zitokanazo na biashara hiyo.

Tupe taarifa kuna matapeli ndani ya minoa kutoa pesa kwa madalali marufuku, kila mwenye nyumba amlipe dalali kwa yule mwananchi atakayeona atoe taarifa ili tuweze kuchukua hatua lakini pia wenye nyumba wasilazimishe miezi 3 au 6 kodi waweke mkataba wa mwezi mmoja  ambao mwananchi ataweza kulipa.

Lukuvi

Aidha ametoa wito kwa wananchi kutumia kituo hicho cha huduma kwa mteja  kwa kutoa malalamiko waliyonayo ikiwa ni pamoja na  kuwafichua waovu ndani ya Sekta ya Ardhi.

“Siyo lazima watu wafunge safari kutoka mkoa mwingine kuja hapa Dodoma akiwa na changamoto yake kituo hiki kitakuwa wazi mwananchi atapiga simu na kutuma ujumbe kupitia 0739-646885 atatoa malalamiko yake au changamoto aliyonayo atatuma navielelezo kupitia watsap “amesema Lukuvi

Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi amesema kuwa taarifa ya migogoro ya vijiji 975 imetolewa maamuzi na baraza la mawaziri ambapo hivi sasa wametuma timu ya wataalam katika vijiji 55  ambavyo vilikuwa na migogoro ya mipaka ili kutatua tatizo hilo .

 



 

Post a Comment

0 Comments