WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII WAPATIWA MAFUNZO



📌DOREEN ALOYCE

WAHUDUMU wa Afya ngazi ya Jamii wamesema kupitia mafunzo mbalimbali wanayoyapata imesaidia kubadilisha mtazamo Hasi  juu ya chanjo ya Covidi 19 na Ugonjwa wa Kifua kifuu TB na changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo kutopewa ushirikiano wa kutosha.

Hayo yaliyabainisha Jijini Dodoma wakati walipokuwa kwenye mafunzo ambayo yamewezeshwa na Shirika la Steps Tanzania kwa ufadhiri wa  Amref fedha kutoka mfuko wa Dunia Global fund  kwa ajili ya kujenga uwezo kwa watoa huduma wa afya ya msingi Community health weakers.

Jane Frank  Mhudumu kutoka Kata ya Makole Jijini hapa alisema kuwa hapo awali Jamii haikuwa na ushirikiano pale walifika Kutoa elimu juu ya Chanjo ambapo walikumbana na maswali yaliyopelekea kukatisha tamaa.

Tunashukuru Shirika la Steps Tanzania kwa elimu hii tutaenda kuwaibua wenye ugonjwa wa Kifua kikuu na kuwapa rufaa kwenda kupatiwa tiba wananchi wetu ni wabishi hivyo l elimu hii itatusaidia kupunguza maswali ,wasiwasi kutoka kwa Wananchi kwani tayari tunapata mbinu mbalimbali

"  Wananchi ni wabishi licha ya kuwaelimisha wamekuwa na wasiwasi wakiuliza maswali na wengine wakiwazuia ndugu zao kupata chanjo lakini kadri tunavyopewa elimu tunapata mbinu mbalimbali za kuwaelimisha na siku hizi wameelimika na kuhamasishana ."Alisema Jane.

Nae Maiga Patroba mhudumu kutoka Kata ya Nkuhungu  alisema kuwa changamoto hapo awali ilikuwa ni kutopewa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Wananchi na Uongozi wa mtaa ikiwemo uvumi kupitia mitandao ya kijamii.

Mratibu wa Huduma za afya ngazi ya Jamii ,Marry Kongola kutoka Ofsi ya mganga Mkuu wa Mkoa amesema mafunzo hayo ni njia ya kuwakumbusha watoa huduma kutambua wajibu wao Katika Kutoa elimu juu ya Chanjo na wenye kifua kikuu.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Steps Tanzania Dkt Cyprian Magere Amesema Shirika Hilo linatekeleza Afua za afya ya Jamii hususani Kuzuia maambukizi ya virus vya ukimwi na kifuu kwa kulenga watu  wenye magonjwa Sugu, walemavu na makundi maalumu Katika Jamii ambayo yako Katika hatari zaidi ya kupata maambukizi hayo nakuwataka wananchi kujitokeza kupata Kinga.

Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wahudumu wa afya ngazi ya Jamii kupata elimu na stadi za kuibua na kuhamasisha wananchi waweze kupata chanjo ya UVIKO 19 na kuibua wagonjwa wapya wa TB sambamba na kurudisha wale walioacha matibabu kutokana na hofu ya Ugonjwa wa Corona.

Alisema  mwitikio wa chanjo ya Covidi 19 ni mkubwa ukilinganisha na kipindi Cha nyuma  kutokana na elimu wanayoitoa na kwamba matarajio ni kufikia Halmashauri nyingine zikiwemo Halmashauri ya Chemba na Chemba ili kupata stadi za kuwaibua wagonjwa wa TB na kuhamasisha watu kupata chanjo .

"Tuna Imani kubwa kupitia mafunzo haya yataenda kuleta tija kwa jamii hasa kipindi hiki tunachoendelea kupambana nacho elimu hii mkaitumie ipasavyo kuwasaidia  niwaombe wananchi msiache kuchukua tahadhari"alisema Bugere .

Post a Comment

0 Comments