WAZIRI MHAGAMA ATAKIWA WATUMISHI KUSIMAMIA MAJUKUMU YAO KWA UFANISI

 


📌RHODA SIMBA


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge Vijana,Ajira na Wenye Ulemevu Jenista Mhagama amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kusimamia Majukumu yao kwa ufanisi , kutekeza program kwa Kila idara pamoja na kutumia maarifa waliyonayo Katika kuleta mafanikio.

Kauli hiyo ameitoa leo January 5 jijini hapa katika kikao na wafanyakazi wa Ofisi hiyo pamoja na Taasisi zake kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yakiwemo mafanikio yaliyojitokeza katika kipindi cha mwaka 2021.

Aidha Mhagama amesema kuwa Katika kufanikisha kusudi la Serikali  wafanyakazi hao wanapaswa  kudumisha mshikamano ,uwajibikaji wa pamoja Katika kutekeleza Majukumu ,uaminifu huku wakitumia hekima na busara kwenye utendaji kazi wao.

"Pia niwatake kuendelea Kupambana  na rushwa na vitendo ambavyo haviendani na utumishi wa umma badala yake mtumie busara ,hekima Katika ufanisi wa kazi huku mkiwa wawazi kutafuta haki zenu kusiko Kuwa na malalamishi ambayo hayana tija "amesema Jenesta.

Amesema kuwa Wizara imeweza kufanikiwa mambo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyuo sita vya watu wenye ulemevu ambavyo vitasaidia  kuweza kuboresha ujuzi na kuboresha maisha yao ya Kila siku huku Serikali ikitenga Bilioni Tisa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la msajili wa vyama vya siasa.

"Pia tumepokea fedha Bilioni 2.5 kwa ajili ya ujenzi wa Tume ya usuluhishi na usimamizi, kituo chenye sura ya kimataifa ni niwatake  mtakaosimamia  ujenzi huo kuwa makini ili jengo liwe imara na Hali ya juu ,

"Na tumepokea Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda Cha kipya Cha kisasa Cha kupiga chapa ambacho kitakidhi vigezo na kusaidia Serikali kufanya kazi kwa Viwango vya juu" amesema Mhagama.

Kwa upande wake Katibu wa Wizara hiyo Tixon Nzunda amesema kuwa kutokana na maelekezo ya Waziri kupitia Ofsi yake watayafanyia kazi huku akiwataka watumishi kuonesha Umoja na mshikamano ili waweze kutimiza malengo yao.

"Tumefaanya maboresho mbalimbali Sekta ya hifadhi za Jamii na uwekeji wa mifumo ambayo itarahisha wanachama kupata huduma Kwa urahisi bila ubaguzi wowote kwani wote ni Ofsi moja"amesema Tixon.

Awali wakitoa kero zao mbele ya waziri Mhagama wajumbe wa kikao hicho walisema Serikali kupitia Ofsi yake wanapaswa kuendelea kuboresha maslahi ya watumishi na kuweka mazingira rafiki ya kutatua changamoto zao.

Pia waliomba kuwepo mafunzo maalumu ya kuwaandaa watumishi kabla ya kustaafu ambayo yatawasaidia kukabiliana na maisha wanapo staafu kwani Wengi wao huwa wanakumbana na changamoto wanapomaliza muda wao wa kazi kwa kukosa elimu hiyo.

Hata hivyo wameiomba Serikali kupitia Ofisi ya waziri mkuu  kushughulikia watu wenye ulemavu wapatiwe viwanja kwa riba nafuu kwa ajili ya kuweka Makazi yao  ambayo wataweza kulipa taratibu.

Post a Comment

0 Comments