ASILIMIA 5 YA MAPATO YA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI HUPOTEA KWA UFISADI



📌
JASMINE SHAMWEPU

RIPOTI ya Kimataifa ya mwaka 2021 iliyotolewa na Taasisi ya taaluma ya kudhibiti Ufisadi Duniani (ACFC ) inasema asilimia 5 ya mapato yanapotea kwa ufisadi kwenye taasisi zote za Umma na binafsi.

Hayo yemesemwa leo jijini Dodoma na Shakibu Mussa Nsekela Bingwa katika masuala ya Ubadhilifu Kudhibiti Rushwa na Ufisadi katika mafunzo ya kuwajengea uwezo taasisi za umma na binafsi kuweza kudhibiti ufisadi katika maeneo yao.

Amesema katika utendaji kazi wao wamebaini kuwa ufisadi unaosikika ni ule unaosikika au kujulikana na ufisadi mwingi haugunduliki au wahusika kuelewana wenyewe kwa wenyewe na kupotea.

Amesema unapotokea ufisadi taasisi hutumia gharama kubwa namna ya kufanya uchunguzi ukaguzi na pesa zilizochukuliwa kuzirudisha inakuwa ni changamoto. 

Tumeona njia bora ya kudhibiti ufisadi ni kuzuia ufisadi usitoke na inapotokea tujenge taswira na  wahusika ipo siku watagundulika, kuwepo na nia ya kuwatafuta watu kuwafatilia ili wagundulike amesema

Na kuongeza kuwa

Kazi yetu kubwa tunawajengea uwezo taasisi za umma na binafsi juu ya dalili za ufisadi namna gani zinatokea na jinsi ya kuthibiti ufisadi 
 Nsekela

Kwa upande wake Dkt Clement Mashamba wakili wa kujitegemea na Mhadhiri wa sheria mwandamizi amesema tatizo la ufisadi ni kubwa kwani watu wengi wanaamini kuwa ili uweze kuwa tajiri lazima ufanye ufisadi lakini pia zipo sababu za kusababisha tatizo hilo liwepo.

Amesema ufisadi unatokea kwa sababu kuna fursa za kufanya hivyo watu wanashinikizio na tatu kuwepo kwa mianya na fursa kwa watu kufanya ufisadi.

Watu wamekuwa wakivunja sheria na taratibu zilizowekwa lakini usimamizi ni mdogo hali inayopelekea ufisadi kuendelea kutokea kikubwa tuangalie upya sheria zetu ili ziweze kubana mianya ya ufisadi na mambo yanayoibuka mapya katika ufisadi kwani sasa ufisadi upo kwenye njia za kidigitali /mitandao 

Naye Meshaki Shashi Kaimu mkuu wa idara ya uchunguzi wa ndani Benki ya Taifa ya biashara  NBC amesema mafunzo hayo ni muhimu kwao kwani yanawaweka pamoja ili na wao kwa umoja wao waende kupambana na ufisadi katika maeneo ya taasisi za umma na binafsi.

Ufisadi ni tatizo kubwa sio kwenye mabenki tu sehemu zote lakini kwenye benki yangu ya NBC ipo kama taasisi na ndio maana tupo hapa katika kuhakikisha tunapeana uwezo kudhibiti uhalifu huu 


Post a Comment

0 Comments