DKT. CHAULA AZITAKA NGOs KUWAJIBIKA KWA WANANCHI


 ðŸ“ŒWMJJWM

KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kufanya kazi ya kuhudumia jamii kulingana na katiba zao, mikataba  na vibali vya kutekeleza miradi kama ilivyoidhinishwa na Msajili wa NGOs.

Dkt. Chaula ameyasema hayo wakati akizungumza na wawakilishi wa Mashirika hayo kutoka Mikoa ya Dodoma, Iringa, na Singida leo Jijini Dodoma ameyahakikishia Mashirika hayo kuwa, atayatembelea kwa kuanza na Mkoa wa Dodoma ili kuhakiki utendaji wao.

Amesema katika kuwasaidia wananchi, mchango wa kila mmoja kati ya Serikali na wadau unahitajika hivyo ni vema kutengeneza misingi ya uwajibikaji kwa pamoja.

Ni ukweli usipingika kuwa mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa na mchango mkubwa katika kuchangia kuleta maendeleo
Dkt Chaula.

"Tunaishi kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, Wizara yetu ni mpya kwa jina lakini majukumu ni yaleyale na yanaeleweka. Wote tunawajibu kwa sababu tunategemeana" ameongeza Dkt. Chaula.


Aidha, Dkt. Chaula amemtaka Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali NaCoNGO kuhakikisha Mashirika 170 ambayo yamesajiliwa Mkoani Dodoma na hayafanyi kazi ambayo ni sawa na  asilimia 47 ya Mashirika 358 yaliyopo Mkoani hapa watafutwe ili kujua wanafanya nini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa NaCoNGO Dkt. Lilian Badi amemuhakikishia Katibu Mkuu kufanya kazi kwa ushirikiano kati ya NaCoNGO na Serikali katika kufuata sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya uendeshaji wa Mashirika hapa nchini.


Awali akitoa taarifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Dodoma, Msajili Msaidizi wa NGOs Mkoa wa Dodoma, Masa Mbasa amesema mkoa huo una jumla ya Mashirika 358 na 188 ndiyo yanafanya kazi sawa na asilimia 53 ya Mashirika yote.

Naye, Mbunge wa Viti Maalum na mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii  Neema Rugangira  ameiomba Serikali kuratibu uwezekano wa kuzijengea  uwezo NGOs ndogo sambamba na kuwapa elimu ya Kodi kwani nyingi zinashindwa kutekeleza jukumu hilo kwa kukosa uelewa. 


Sheria ya NGOs ya Na. ya mwaka 2019 inayohimiza uwazi na uwajibikaji iliwekwa ili sekta hii iratibiwe na kufanya kazi kwa ufanisi ili iweze kusaidia kuchangia katika jitahada za Serikali kutatua changamoto za wananchi katika maeneo yao
Neema Rugangira.

Nao baadhi ya washiriki wakizungumza kwa niaba ya NGOs amesema ni muhimu kushirikisha Serikali katika ngazi zote kuanzia Wizara hadi Halmashauri katika shughuli zote wanazofanya kuhudumia Jamii ili kuweza kuimarisha utekelezaji na kuhakikisha ufanisi wa kazi pamoja na kuwezesha Jamii kumiliki miradi inayotekelezwa.

 

Post a Comment

0 Comments