DKT. GWAJIMA APOKEA UGENI WA ‘UN WOMEN’, WAONESHA UTAYARI KUBORESHA MIONGOZO YA WIZARA

 


📌WMJJWM

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaum, Dkt. Dorothy Gwajima, amepokea ugeni wa Shirika la kupigania haki za wananawake na usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi, UN Women, na kuweka mikakati ya pamoja katika kufanya kazi na kuwahudumia wanatanzania katika masuala ya usawa wa kijinsia.

Ugeni huo kutoka UN Women, ukiwa umeongozwa na Mwakilishi Mkaazi, Hodan Addou pamoja na Mkuu wa masuala ya maendeleo kutoka nchini Finland Timo Voipio, ulimuelezea Waziri Gwajima, dhamira ya Shirika hilo, kusaidiana na Serikali katika msuala ya usawa wa kijinsia kwenye uongozi hususan ni ngazi za jamii kwenye Serikali za Mitaa.

Akizungumza katika kikao hicho Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameuambia ujumbe huo kuwa, kama Wizara wapo tayari kufanya kazi na shirika hilo hasa kwa upande wa vipaumbele ambayo Wizara imejiwekea ikiwepo kukuza usawa wa kijinsia kwa viongozi katika ngazi jamii ambapo tatizo limeoneka kuwa kubwa ikilinganishwa katika ngazi ya Mikoa na Taifa. 

Dkt. Gwajima ameongeza kuwa kwa sasa Wizara inaandaa taarifa ambayo itawasilishwa nchini Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, ambapo taarifa hiyo itaangazia athari za hali ya mabadiliko ya tabia nchi na kwa namna gani wanawake wa watanzania wamejipanga kupambana na hali ya mabadiliko ya nchi sambamba na masuala ya uongozi na usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi.

Chini ya Uongozi wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, tumepiga hatua kwa nafasi za wanawake ngazi za juu, lakini kama Wizara tunataka elimu hiyo, ifike ngazi za jamii ambako bado uelewa bado upo chini, hivyo kupitia Shirika lenu la UN Women tunaimani tutafanikiwa katika hili
Dkt. Gwajima.

Kwa upande wake Meneja wa Programu katika kuwainua wanawake, Lilian Mwamdanga, kutoka Un Women, aliyekuwa ameambatana katika ujumbe huo, amesema pamoja na mambo mengine yakuangalia usawa wa kijinsia vilevile wataona namna gani nzuri yakushirikiana na Serikali katika kuangalia baadhi ya Sheria na miongozo.

Kwakuwa hii ni Wizara mpya na Mhe. Waziri umetuelezea uwepo wa baadhi ya Sera zinazomzungumzia mwanamke au mambo ya usawa wa kijinsia lakini kwa namna moja au nyingine zimepitwa na wakati na zingine zipo lakini utekelezaji wake una sura ya kusua sua, hivyo UN Women, tupo tayari kusaidiana kuandaa miongozo mipya itakayokwenda na wakati.
 Liliani.

Pamoja na mambo mengine Shirika hilo la limeahidi kuandaa Semina ndogo kwa viongozi ili kuwapitisha viongozi na watendaji kuweza kupambanua shughuli zao wanazo zifanya hapa nchini kama UN Women ili viongozi na watendaji waseriali waweze kuona fursa zaidi walizonazo.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, imeendelea kupokea wadau mbalimbali wa maendeleo itakaoshirikiana nao katika kutekeleza afua mbalimbali zinazosimamiwa na Wizara hiyo.

 

Post a Comment

0 Comments