EWURA YATANGAZA BEI MPYA ZA MAFUTA KWA BAADHI MIKOA

 


📌JOYCE KASIKI

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)  imetaja  Bei mpya za mafuta aina ya petrol dizel na mafuta ya taa kwa mwezi februari mwaka huu ambapo baadhi ya mikoa imepanda na mikoa mingine kupungua.

Aidha ,kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa bei ya mafuta kwa mwezi Machi na Aprili 2022.

Hayo yamesemwa leo Februar Mosi 2022 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godfrey Chibulunje wakati Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kupandia na kushuka kwa bidhaa hizo kwa baadhi ya mikoa nchini.

Ameswma Bei za rejareja za mafuta ya petroli,dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam,zimepungua kwa shilingi 21 kwa Lita (petroli) na shilingi 44 kwa Lita (mafuta ya taa) wakati Bei ya dizeli imeongezeka kwa shilingi 13 kwa Lita.

Aidha alisema Bei za reja reja kwa mafuta ya petroli na dizeli kwa mikoa ya Kaskazini (Tanga,Kilimanjaro,Arusha na Manyara)zimepungua kwa shilingi 123 kwa Lita (petroli) na shilingi 92 kwa Lita (dezeli mtawalia)huku akisema kutokana na kumalizia kwa mafuta ya taa kwenye maghala ya kuhifadhia yaliyopo Tanga .

Amewataka waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kaskazini kuchukua mafuta ya taa kutoka Bandari ya Dar es salaam ili Bei za mafuta ya taa katika mikoa hiyo zilingane na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.

Mhandisi Chibulunje amesema Bei za rejareja za mafuta ya petroli na dizeli kwa mikoa ya Kusaini (Mtwara,Lindi na Ruvuma) zitaendelea kuwa zile zilizotangazwa January 5 mwaka huu huku akisema hiyo ni kwa sababu mwezi January hakuna shehena ya mafuta iliyopokelewa kupitia Bandari ya Mtwara.

Vile vile Mhandisi huyo amesema kwa kuwa hakuna maghala ya kuhifadhia mafuta ya taa katika Bandari ya Mtwara,waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kusaini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika Bandari ya Dar es salaam ili Bei za rejareja za mafuta ya taa ilingane na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.

Mhandisi Chibulunje amesema,katika kuhakikisha kunakuwa na ushindani sawa katika Bei zinazoanza kutumika februuari 2,2022 ,ununuaji wa mafuta kutoka kwenye maghala Sasa kutakuwa na Bei mbili yaani Bei kikomo ambayo muuzaji hatatakiwa kuzidisha na Bei ya chini ambayo muuzaji hatatakiwa kushuka zaidi.

Akizungumzia mwendo wa bei za mafuta kwa mwezi Machi na April mwaka huu amesema,upo uwezekano wa bidhaa hiyo kuongezeka katika soko la dunia.

Hata hivyo amesema Ewura inaendelea kufuatilia mwendo huo kwa karibu ili kuishauri Serikali hatua za kuchukua katika harakati za kupunguza makali ya Bei za mafuta katika kipindi hicho.

Post a Comment

0 Comments