JIJI LA DODOMA LATOA MIKOPO YA FUSO,BAJAJI,GUTA NA BODABODA KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI 📌PENDO MANGALA

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imekabidhi vifaa mbalimbali kwa vikundi vya ujasiliamali ikiwa ni pamoja na lori aina ya fuso tani saba kwa ajili ya kubebea mchanga na matofali, ikiwa ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ambayo yanatakiwa kurejeshwa kama mkopo kwa Vijana, Wanawake, na Watu Wenye Ulemavu.

Akikabidhi mikopo hiyo mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amesema kuwa mikopo hiyo ni kwa ajili ya shughuli za viwanda,Guta 1,Lori moja la kubebea tofari na mchanga,fuso tani saba na mikopo kwa ajili ya biashasha ndogondogo, mikopo ya kilimo,mikopo ya mifugo na mikopo kwa ajili ya mama lishe na baba lishe.

Shekimweri alisema kuwa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha halmashauri ya Jiji la Dodoma imeweza kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi 817,400,000 kwa vikundi 78 vilivyokabidhiwa hundi leo.

Mikopo hii itimike katika kuwaletea maendeleo ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja,jamii inayomzunguka pamoja na taifa kwa ujumla kwa kutimiza niya ya serikali ya kukuza uchumi wa mtu na uchumi wa vitu
DC Shekimweri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji hilo Joseph Mafuru ameema kuwa, katika kutekeleza sera ya kutoa asilimia kumi katika makundi ya vijana,akina mama na makundi maalumu halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kipindi cha mwaka wa fedha imetoa jumla ya mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8.87.
Taarifa inaonesha kwamba shilingi 3,981,070,933.62 tu ndizo zimerejeshwa ambapo ni sawa na asilimia 44.9 ya kiasi kilichotolewa cha mikopo iliyotolewa
Mkurugenzi Mafuru amesema kuwa katika mikopo iliyotolewa leo kwa upande wa vikundi 46 vya wanawake wamepata sh.395,000,000 ,vikundi 23 vya vijana wamepata sh.364,000,000 na vikundi 19 vya watu wenye ulemavu wamepata sh.58,400,000 na kufanya jumla ya vikundi 78 kupata jumla ya fedha sh.817,400,000.

Naye Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde aliwataka wanavikundi wote wanaonufaika na mikopo hiyo kuitumia kwa lengo lililokusudiwa huku akiimwagia sifa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kutekelezwa kwa kiwango kikubwa takwa hilo la kisera la kutoa asilimia kumi ya  mapato ya ndani kwa makundi hayo.

Akitoa ushuhuda, mwenyekiti wa kikundi cha Ilumbo Group ambacho kilishanufaika na utaratibu huo Monica Masado alisema kikundi hicho kimekuwa wanufaika wakuu wa mikopo kutoka katika halmashuri ya Jiji la Dodoma.

Monica amesema kuwa mikopo hiyo ambayo inatolewa na halmashauri ya Jiji imeweza kuinua maisha ya watu pamoja familia zao.
Hata hivyo amesema wakopaji wanaokopa wanatakiwa kuhakikisha wanakopa na kurejesha kwa wakati.

Naibu Meya wa Jiji la Dodoma Emmanuel Chibago aliwataka wakopaji kufanya shughuli za maendeleo badala ya kukopa na kutumia fedha hizo kwa shughuli tofauti na makusudio ya kikundi jambo ambalo linaweza kusababisha kushindwa kufanya marejesho ili vikundi vingi zaidi viweze kukopeshwa na Halmashauri hiyo

Post a Comment

0 Comments