PROF. SHEMDOE: UWEZO WA BAADHI YA HALMASHAURI KUTOITEGEMEA SERIKALI KUU WAPANDA

 


📌RHODA SIMBA

KATIBU  Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)   Prof. Riziki Shemdoe amesema katika kipindi cha miaka 4 iliyopita  kupitia utekelezaji wa Mpango wa Usimaminzi wa fedha za Umma (PFMRP) awamu ya 5  baadhi ya halmashauri zimepunguza utegemezi wa fedha kutoka Serikali kuu kutokana na ongezeko la matumizi sahihi ya  makusanyo ya mapato.

Akizungumza leo jijini hapa februari 25 na wadau wa Menejimenti ya fedha za umma wakati wa kikao cha Kamati ya utekelezaji wa mpango huo, Katibu Mkuu Prof. Shemdoe amesema kuwa baadhi ya halmashauri zimeweza kusimama bila msaada wa serikali kuu kwa  asilimia 25%.

Mpango wa PFMRP unafadhiliwa na Uingereza kupitia Ofisi ya Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya kigeni (FCDO) ukiwa na malengo mahususi ya kuleta mageuzi katika usimamizi  fedha za umma na mradi huo wa miaka mitano utakoma mwishoni mwa mwaka huu wa fedha.

Prof.Shemdoe ameeleza kuwa kabla ya mpango huo mwaka 2016  kuwa rekodi zinaonyesha  halmashauri zinaweza kuendelea bila Serikali kuu kwa asilimia 8 lakini sasa ufadhili wa kujitegemea ulipanda hadi asilimia 15 huku halmashauri za miji kama Temeke au Ilala zikifikia 25%.

 

Post a Comment

0 Comments