UNAONGEA MUDA MREFU NA SIMU? UNALALA KARIBU NA SIMU? : TUME YA MIONZI YATOA TAHADHARI



📌RHODA SIMBA

TUME ya nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imeitaka  jamii kuachana na tabia ya kuongea  kwa muda mrefu,kulala karibu na simu ili kuepukana na madhara yatokanayo na mionzi iliyopo kwenye simu hizo.

Hayo yamesemwa leo Februari 14 jijini hapa, na Mkurugenzi  wa  TAEC Profesa Lazaro Busagala katika kikao cha wadau kilicholenga kupitia kanuni za ada,tozo na mapendekezo kwa wafanyabiashara wenye vifaa vya mionzi ambapo alisema mionzi itakonayo na simu inaathari kubwa katika afya ya mwanadamu ikiwemo kuvurugika kwa ubongo.

Kadhalika amewataka watu ambao wanatumia vyanzo vya mionzi kuzingatia na kufuata masharti waliyopewa na Tume hiyo kwani mionzi inaweza kusababisha madhara  katika afya ya mwanadamu ikiwemo kupata saratani.

Ni kwamba tabia ya mionzi huwezi ukaiona wala huwezi kuinusa  hata kuhisi ila inatambulika kwa  vifaa maalumu  na kwa vipimo vyetu mpaka sasa niwaambie tu wananchi Serikali yao kupitia Tume  inafanya kazi vizuri na wananchi wapo salama mpaka sasa hivi.

Pia mkurugenzi huyo amewataka wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusu na vifaa vya mionzi vinavyotumika hospitali kama vifaa tiba,alisema ukaguzi walioufanya wamelizishwa na usalama wake.

“Matumizi mbalimbali yanayohusiana na mionzi  tuna kaguzi za kushtukiza na zile za kupanga, mpka sasa hivi wananchi waende hospitali wawe na amani vifaa vipo salama kwasababu hata hizo sehemu ambazo vifaa vyao havipo vizuri tulishavifungia nizidi kuwasisitiza tu kwamba tupo salama”amesema Busagala

Amesema katika mionzi kuna madhara ya papo kwa hapo na jamii mara nyingi imekuwa  ikiyapuuza  na kuwataka wale ambao tayari  wamepewa leseni  ya kuweza kutumia vitu hivyo vyenye mionzi kuzingatia.

Tupo hapa kwaajili ya kulinda wananchi na  kuboresha biashara  zao hata watakaposafirisha  kwenda nje ya nchi viwe salama, ili tuweze kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na  kwa taifa kwa ujumla,

“Mionzi inaweza kutumiwa vizuri hasa kwa wale wanaopeleka vyakula nje ya nchi wasije poteza biashara, Nguvu ya tume za atomiki kwanza imejidhatiti kuhakikisha kwamba inasogeza huduma kwa wananchi kwa uharaka na urahisi”amesema Busagala.

 

Post a Comment

0 Comments