WASIOLIPA KODI YA PANGO LA ARDHI WAPEWA SIKU 60

 


📌RHODA SIMBA

WIZARA ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa siku 60 kwa wale ambao hawajalipa  kodi ya pango la ardhi na waliopimiwa viwanja na hawajamilikishwa  kuwasilisha maombi ya kumilikishwa viwanja na wasipofanya hivyo   Serikali itachukua hatua za  kisheria ikiwemo kufuta umiliki,kupiga mnada na kumilikisha viwanja  vilivyopimwa kwa wananchi wengine wenye uhitaji.

Hayo yamesemwa leo Februari 24,na Afisa Ardhi Mkuu kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Biswalo Makwasa wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu umiliki ardhi kwa viwanja vilivyopimwa pamoja na ulipaji wa kodi ya pango la ardhi.

Amesema wamiliki wa ardhi wanakumbushwa wajibu wao wa kisheria wa kulipa kodi ya pango la ardhi.

Wizara inatoa muda wa siku 60 kuanzia tarehe 5 mwezi wa pili 2022 ya kuhakikisha wale walipopimiwa viwanja wanawasilisha maombi  ya kumilikishwa  na wale wenye milki za ardhi wawe wamelipa kodi ya pango la ardhi

Amesema mmiliki ambaye hatalipa kodi Serikali itachukua hatua za  kisheria ikiwemo kufuta umiliki,kupiga mnada na kumilikisha viwanja  vilivyopimwa kwa wananchi wengine wenye uhitaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Denis Mesamu  ametoa rai kwa watanzania kulipa kodi ya pango la ardhi kwa njia ya kieletroniki kwa kutumia simu  kwani ni rahisi na ni rafiki.

bado kumekuwa na changamoto kwa watanzania kushindwa  kutofautisha kati ya  kodi ya pango la ardhi na kodi ya majengo,kodi ya majengo  inakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kwa sasa  inakusanywa  kupitia luku kwenye umeme.

Amesema   kodi ya pango la ardhi inakusanywa na Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia mifumo ya Kieletroniki hivyo amewaomba wananchi anaedaiwa kodi hiyo kulipe.

Pia amesema Wizara ina mkakati wa kwenda nyumba kwa nyumba kuhakikisha kila kipande cha ardhi kinachodaiwa tunakipelekea hati ya madai ambapo amedai hali hiyo inaleta tija.

Amesema kwa Mkoa wa Dodoma ulipaji wa kodi ya ardhi umeongezeka ambapo katika kipindi cha Disemba mwaka jana wiki mbili za kwanza ulipaji wa kodi ulikikuwa wamiliki 200 lakini baada ya kuanza zoezi la kupeleka hati za madai walifika mpaka 200 kwa wiki na mapato yalitoka shilingi milioni 40 kwa wiki mpaka milioni 102.

 

Post a Comment

0 Comments