WAZIRI KIJAJI AWATAKA WAFANYABIASHARA KUPUNGUZA BEI VIFAA VYA UJENZI

 

📌DOREEN ALOYCE

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Ashatu Kijaji amewataka wazalishaji wa vifaa vya ujenzi,wasambazaji na wafanyabiashara kushusha mara moja Bei za bidhaa hizo walizopandisha kiholela bila sababu za msingi ambayo imepelekea kumuumiza mlaji wa Chini.

Agizo hilo ni matokeo ya tathimini ilibaini masuala kuwa na ongezeko holela wa vifaa vya ujenzi  hususani saruji na nondo ambalo linasabishwa na wazalishwaji wa bidhaa husika kufanya uzalishaji banifu na kutokuwa na mfumo wa wazi.

Waziri Kijaji ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati alipokuwa akiongea na vyombo vya Habari ambapo pia alisema agizo hilo pia  linawahusu wazalishaji na wasambazaji wa vinywaji baridi.

Amesema kuwa tathimini ilijiridhisha kuwa gharama halisi za uzalishaji wa saruji haiakisiwi Katika bei ya saruji iliyopo sokoni ikilinganisha na uwiano huo Katika Nchi jirani, na kwamba ongezeko wa Bei ya Saruji na nondo halina uwiano halisi na gharama za usafirishaji na usambazaji.

Utafiti wetu umegundua kuwa kuna ucheleweshaji wa makusudi kwa utoaji wa saruji kutoka viwandani kwenda kwa wasambazaji na wanunuzi wa ndani hususani wale wasambazaji na wanunuzi wadogo ambao tayari wanakuwa wamekwisha lipia saruji husika na kuweza kusababisha wao kupandisha bei 
Kijaji 

Aidha kupitia utafiti huo Kutoa maagizo  mamlaka zote za udhibiti kuchukua hatua Kali dhidi ya walimbikizaji na wauzaji kupitia mlango wa nyuma(black market)wanaosababisha bei za bidhaa kupanda sokoni ili kuhakikisha Bei zinafika sokoni Kwa wakati na kwa bei shindani ambayo haina maumivu kwa wananchi.

Kwa kuwa kitendo cha kupanga bei kati ya washindani ni uhujumu uchumi nawaagiza mamlaka husika kuchukua hatua Kali dhidi ya wote wataobainika kukaa na kupanga bei kwa bidhaa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu

"Ninawaelekeza wazalishaji kuzalisha bidhaa hizo kulingana na uwezo uliosimikwa kwenye viwanda vyenu ili kukidhi mahitaji ya Soko ndani ya Taifa letu na kuwa na uwezo wa kuuza nje ya mipaka yetu ."amesema Kijaji 

Pia wazalisha wa vifaa vya ujenzi kuhakikisha wanaweka mifumo mizuri ya usambazaji wa vifaa ili Kuzuia kupanda kwa bei huku akiwataka maafsa biashara wa Mikoa na Wilaya kote Nchini kufuatilia kwa karibu mwenendo wa Bei za bidhaa kwenye maeneo yao na kuwasisha taarifa mara kwa mara .

Hata hivyo amesema Serikali ina wajibu wa kidhibiti mienendo hadhaifu na kandamizi ya wazalishaji wa bidhaa,wafanyabiasha kwenye soko ikiwa ni pamoja na upandishaji holela wa Bei zote Nchini huku mwenye nia ovu ya kumkandamiza mwananchi kuchukuliwa hatua .

 

Post a Comment

0 Comments