ALIYETAMANI CHEO CHA IGP AHAMISHIWA MAKAO MAKUU DODOMA


📌MARIA ROBERT

 

KAMISHNA Msaidizi wa Polisi (ACP)Wankyo Nyigesa  ambaye alipangiwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera,amehamishiwa Makao Makuu ya jeshi la Polisi Dodoma ili kupisha uchunguzi wa kauli yake aliyoitoa wakati wa hafla ya kumuaga mkoani Pwani.

Akizungumza Kibaha Mkoani Pwani wakati wa kumuaga baada ya uhamisho katika mkoa, Nyigesa alisema moja ya malengo yake na ndoto zake kubwa ni kuteuliwa kuwa Mkuu wa Polisi nchini (IGP) na anatamani Rais amteue huku akiahidi kuwa atafanya kazi kubwa.

Siku moja tafadhali niteue kuwa IGP, mimi naamini nitafanya makubwa, huwa ninaomba sana Mama (Rais) siku moja aniote tu halafu anitamke tu niwe IGP, Mimi nitamuomba nifanye miaka mitatu halafu nimwambie Mama mimi nakukabidhi naondoka unaonaje hapo
ACP Nyigesa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (29/03/2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi,SACP David Misime imesema (ACP)Wankyo Nyigesa amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma kutoka kuwa RPC Kagera..

"Uhamisho huu umefanyika ili kupisha uchaguzi wa tukio lililofanyika machi 23,2022 kwenye sherehe ya kumuaga aliye kuwa kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ambapo alitoa maneno yanayoonyesha ukiukwaji wa nidhamu kulingana na miongozo ya jeshi la polisi.

"Suala hilo  limeanza kufanyiwa kazi na matokeo ya uchunguzi huo yatafanyika katika mamlaka za kinadhamu kwa hatua zaidi,"imesema taarifa.

Pia taarifa hiyo imesema Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro amefanya uhamisho na mabadiliko kwa baadhi ya makamanda polisi wa mikoa nchini, aliye kuwa mkuu wa Operesheni mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mashenene Mayila anakuwa afisa Mnadhimu mkoa wa Rukwa.

 Aidha Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) William Mwampangale amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera na  nafasi yake imechukuliwa na aliye kuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa huo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Theopista Mallya.

 

 

Post a Comment

0 Comments