CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA-HOMBOLO CHATENGA 550M/- KUBORESHA MIUNDOMBINU

 


📌MARIA ROBERT (DOMECO)

CHUO cha Serikali za Mitaa (LGTI-Hombolo) kimetenga kiasi cha shilingi milioni 550/- kwa ajili ya kwaajili ya ukarabati wa miundo mbinu na majengo mbalimbali ikiwemo mabweni ya wanafunzi, nyumba za watumishi na mifumo ya maji safi na maji taka.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa Chuo hicho Dkt.Mpamila Madale wakati akielezea mafanikio ya chuo hicho katika kipindi cha mwaka mmoja mmoja wa sSerikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Dkt.Madale amesema kuwa mpaka sasa ukarabati huo unaohusisha pia nyumba 10 za Watumishi na Mabweni 7 ya Wanafunzi umefikia asilimia 65%.

Ujenzi huo utatumia jumla ya shilingi milioni 350 na hadi sasa tumepokea zaidi ya shilingi milioni 907 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa awamu ya kwanza katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa serikali ya awamu ya sita na ukamilikaji wa jengo hilo utaongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya taasisi.

Pia Dkt.Madale ameishukuru serikali awamu ya sita kwa kuipatia taasisi hiyo eneo lililokuwa ofisi ya zamani ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ili litumike kujenga ‘kampasi’ kubwa na ya kisasa na amebainisha kuwa chou kimetenga kiasi cha shilingi milioni 255/- kwa hatua za mwanzo wa utekelezaji wa ujenzi huo.

Aidha amesema kuwa katika kuhakikisha chuo  hicho kinaongeza wigo wa elimu nchini wapo kwenye hatua za kuanzisha kampasi nyingine Zanzibar.

Uanzishwaji wa serikali za mitaa kampasi hii ya Zanzibar itakuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi na watumishi wa Zanzibar na maeneo ya Jirani

Aidha amesema kuwa chuo hicho kimekuwa na ushirikiano mzuri na Taasisi kadhaa za kitaifa na kimataifa na kutoa mafunzo na semina mbalimbali kwa watumishi wa kada mbalimbali ya serikali za mitaa.

"Chuo  kimefanya jumla ya mafunzo ya washiriki 636 ikijumuisha watendaji wa mitaa na wajumbe wa kamati ya mitaa na kwa ufadhili wa UNICEF chuo pia kimeendesha mafunzo kwa wenyeviti wa kamati za huduma 3 za halmashauri 16 kutoka mikoa ya Dodoma, Singida,Iringa,Songwe,Njombe na Mbeya ambapo jumla ya washiriki 48 walinufaika," alisema.

Pia amesema katika kipindi cha mwaka 2021/2022 Chuo hicho kimefanikiwa kuongeza Udahili na kuwa na jumla ya Wanafunzi 6,066 ambapo kati yao Wanawake ni 3367 na Wanaume ni 2699.

 

 

 

Post a Comment

0 Comments