DKT. CHAULA AIOMBA TBA KUHARAKISHA MCHORO WA JENGO LA WIZARA

 

📌WMJJWM

KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amewaomba Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) kuharakisha taratibu za kupata mchoro wa jengo la Ofisi za Wizara hiyo ili ujenzi uanze mapema.

Dkt. Chaula ametoa kauli hiyo wakati akipokea kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Wizara, katika Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma tangu kuundwa kwa Wizara hiyo mpya ambapo kabla ilikuwa ni sehemu ya Wizara ya Afya.

 Amesema TBA ifanye jukumu lake la kuhakikisha mchakato wa ujenzi unakamilika kwa wakati hivyo kuwezesha Wizara kuendelea kuhudumia wananchi kwa sababu inagusa makundi yote katika jamii ikiwemo makundi maalum.

Kikubwa tunakimbizana na muda, kwa hiyo tumeshakabidhiwa eneo hili, hivyo wenzetu wa TBA watoe michoro ili ujenzi uanze kwani Wizara hii ni mtambuka

Dkt. Chaula 

 Kwa upande wake, Mratibu wa ujenzi wa Mji wa Serikali Meshack Bandawe amesema kutokana na mahitaji ya Wizara hiyo kwa ukubwa wake kulikuwa na umuhimu wa kuwa na eneo lake na jengo kamili ili kurahisisha shughuli zake na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi ili kukidhi mahitaji ya Serikali kwa miaka ijayo. 

Kwa hatua hii tunatarajia jengo la Wizara hii litakuwa miongoni mwa majengo 25 yatakayojengwa hapa Mtumba, mara baada ya taratibu za kimamlaka kukamilika

Bandawe.

 Naye Msanifu majengo kutoka TBA Ngh'olo Weja amesema TBA itatahakikisha mchoro wa majengo hayo, unakamilika mapema kwa kufuata sheria pamoja na taratibu zote za kumpata mkandarasi. 



 

 MWISHO

Post a Comment

0 Comments