DR.TAX:ULINZI NA USALAMA NI MUHIMU KWA MAENDELEO YA NCHINI

 


📌HAPPY RICHARD (DOMECO)

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Stergomena Lawrence Tax amesema Ulinzi na Usalama wa nchi ni muhimu katika Maendeleo ya Taifa lolote Duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari akielezea mafanikio ya Wizara katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia,Dkt.Tax amesema Wizara hiyo imejidhatiti kukabiliana na changamoto za kiusalama dhidi ya maadui toka ndani na nje na kuhakikisha kuwa mamlaka na maslahi mapana ya nchi yanakuwa salama.

"Tumendelea kuhakikisha kuwa nchi yetu ipo salama na amani inalindwa kwa kuimarisha umoja,mshikamano na utulivu nchini pia wizara inatoa  shukrani za dhati kwa mheshimiwa Rais kwa kuhakikisha kuwa kiasi cha fedha kilicho tengwa kwa matumizi ya wizara ya ulinzi na JKT na Taasisi kimetolewa kwa zaidi ya asilimia 80 (80℅) na kiasi kilicho salia kinatarajiwa kutolewa kufika mwishoni mwa mwaka huu ",alisema

Dkt.Tax amesema Serikali ya awamu ya sita imeiwezesha wizara ya ulinzi la jeshi la kujenga Taifa kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa weledi,umakini,na mafanikio na hivyo kuiwezesha nchi kuendelea kuwa na amani na utulivu.

Aidha katika kipindi hicho, serikali ya awamu ya sita wizara imewezeshwa kulipa madeni yenye thamani ya zaidi shilingi billioni 175 kwa wazabuni waliotoa huduma mbalimbali hali ambayo imejenga imani kwa serikali na kuiwezesha Wizara kuendesha majukumu yake ya msingi kwa ufanisi.

Pia amesema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita Wizara hiyo kupitia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),imeendelea kuimalisha ulinzi wa mipaka ya nchi yetu na nchi imeendelea kuwa shwari.

Kulikuwepo na changamoto chache katika baadhi ya mipaka, hususani mpaka wa kusini hata hivyo changamoto hizo zimeshughulikiwa ipasavyo na hali ya amani na utulivu imeendelea kutamalaki

Ameendelea kusema kuwa Wizara yake imeweka kushughulikia migogoro ya ardhi ipatayo 74 katika mikoa ya Arusha Chukwani, Dar_es_salam, Dodoma Kagera,Kigoma,Lindi,Mara,Morogoro,Mwanza,Njombe,pwani,Rukwa,Ruvuma,shinyanga,Singida, Tabora na Kisaka huko zanzibar.

Aidha Wizara kupitia chuo cha Ulinzi wa Taifa (National Defence College-NDC) imeendesha mafunzo ya ulinzi na stratejia ya muda mrefu na mfupi kwa maafisa wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na watumishi wa umma.

Alisema mazingira bora ya utendaji kazi ni muhimu, na serikali ya awamu ya sita imeiwezesha Wizara kuendelea na ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi katika eneo la Kikombo Dodoma na ujenzi huo unaotekelezwa kwa kutumia rasilimali fedha na wataalamu wa ndani umefikia asilimia 70 na unatarajia kukamilisha ifikapo June 2022.

Alisema kuwa Wizara kupitia mashirika yake ya Tanzania Automotive Technology Centre (TATC) na MZINGA Imeendelea kufanya utafiti na uhasilishaji wa teknolojia ili kuzalisha bidhaa na huduma mbalimbali kwa matumizi ya kijeshi na kiraia.

Dkt.Tax amesema mafanikio ambayo Wizara imeyapata katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi vimetokana na umahiri na uwezeshaji unaofanywa na serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

 Kupitia kwenu (Waandishi) nitoe wito kwa watanzania wote kuendelea kudumisha amani na utulivu kwa ustawi wa Taifa letu na manufaa yetu sote

 

 

 

Post a Comment

0 Comments