NBS YATOA TAHADHALI TOVUTI YA UZUSHI

 


📌
RHODA SIMBA

OFISI ya Taifa ya Takwimu NBS na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar OCGS imetoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa hadi sasa haijatangaza nafasi za kazi za Makarani wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

Tahadhari hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwepo wa tovuti ambayo inatangaza kuwa nafasi za kazi zimetoka ambapo amesema mpaka sasa NBS na OCGS haijatoa taarifa hizo.

Hivi sasa kuna tovuti yenye jina la https:/www.sensatanzania.com ambayo inatangaza kuwepo kwa nafasi za kazi za Makarani wa Sensa na tayari baadhi ya watu wameshajisajili kwenye mfumo huo kwa malipo,

NBS na OCGS inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa serikali haijaanzisha tovuti rasmi ya sensa hivyo tovuti ya https.//wwwsensatanzania.com. si rasmi hivyo haitambuliwi na Serikali

Chuwa.

 Amesema kuwa nafasi za ukarani na usimamizi wa sensa zitatangazwa rasmi kupitia tovuti na mitandao ya kijamii ya NBS na OCGS baada ya taratibu zote za Serikali zitakapokamilika.

Kazi ya kuwapatia watumishi hao wa sensa itasimamiwa na kamati za sensa za Mkoa ambazo wenyeviti wake ni wakuu wa mikoa husika, Nia ya serikali kufanya hivyo ni kuhakikisha watu wote wanaotaka kufanya kazi za ukarani na usimamizi wa sensa watoke katika maeneo yao wanaoishi,

Kadhalika Dkt. Chuwa amewataka watanzania wenye nia ya  kuomba nafasi hizo kufuatilia Mawasiliano rasmi  ya Serikali ikiwemo tovuti za Ofisi ya taifa  ya Takwimu NBS na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar OCGS.

Watanzania wote wenye nia ya kuomba nafasi hizo wafuatilie Mawasiliano rasmi ya Serikali ikiwemo tovuti za Ofisi ya taifa ya takwimu NBS www.nbs.go.tz na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar OCGS www.ocgs.go.tz, Ofisi za wakuu wa Mikoa, Wilaya,kata na Tarafa. 

Chuwa.

 MWISHO

Post a Comment

0 Comments