SERIKALI KUHARAKISHA UTENGAJI MAENEO KURAHISISHA SENSA

 

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

SERIKALI imekusudia kumaliza zoezi la kutenga maeneo kwa ajili ya kuhesabu watu ifikapo mwishoni mwa mwezi Machi, 2022 lengo likiwa ni  kurahisisha kazi kwa makarani pindi  zoezi  la sensa ya watu na makazi litakapoanza  hapo mwezi Agost 2022.  

Hayo yameelezwa  leo Machi 23 jijini Dodoma na Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara, Bi. Anna Makinda  katika kata ya Chang’ombe wakati akiukabidhi uongozi wa kata hiyo kikosi kazi maalum kwaajili ya utekelezaji wa zoezi hilo.

“Yaani yote tuseme kama maeneo hayajatengwa hatuwezi kuhesabu watu na kama tulivyosema watatumia teknolojia katika kufanya kazi  vishikwambi na hao vijana mnao waona wote hamwafahamu kwahiyo ninyi ndio mnowajibu kama wenyeviti kuwaonesha piteni hapa hapa ndio mwisho wa mtaa wa Mzee fulani” amesema  Makinda

Awali akizungumza Mwenyekiti wa mtaa wa Mazengo Bw. Abdallah Ally amesema kuwa jamii inatakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia zote

Zoezi hili ni muhimu na ndio litakalokuja kuainisha mahitaji ya mtaa idadi ya mtaa ili kupanga majukumu ya kimaendeleo makazi miundombinu hiyo utajua kutokana na  takwimu halisi
Abdallah Ally

Kwa upande wake mrasimu ramani kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Khatibu Kuchengo amesema dhumuni la kufanya zoezi la kutenga maeneo kabla ya kuhesabu watu ni kuepuka muingiliano katika maeneo na mipaka.

“ili kuwasaidia makarani wanapoanzia kufanya zoezi la kuhesabu ni wajue wanaanzia wapi na eneo la kumalizia  ni wapi tofauti  na pakiwa hakuna mpaka ”amesema  Kuchengo

 

Post a Comment

0 Comments