TANAPA YATANGAZA KIFO CHA FARU RAJABU



📌HAPPY RICHARD NA MARIA ROBERT

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imetoa taarifa ya  kifo cha Faru Rajabu mwenye umri wa miaka 43 kilichotokea usiku wa kuamkia leo ndani ya katika hifadhi ya Taifa Serengeti kutokana na sababu ya uzee.

Kwa mujibu wa taarifa Iliyotolewa na kamishna msaidizi mwandamizi (Mawasiliano) wa hifadhi za Taifa Pascal Shelutete imeeleza kuwa Faru Rajabu alikuwa mtoto wa Faru maarufu aliyejulikana kama Faru John aliyefariki mwaka 2015 akiwa na miaka 47, Faru Rajabu ameacha watoto na wajukuu na vitukuu kadhaa.

Kama ilivyo kawaida ,kanuni asili za uhifadhi huona namna bora za kuhifadhi mwili wa faru Rajabu,alizaliwa kqenye eneo ngorongoro mwaka 1979 na ambapo 1993 alihamia katika hifadhi ya serengeti ameacha watoto,wajukuu na vitukuu kadhaa.

Taarifa hiyo imebainisha kwamba wastani wa maisha ya Faru weusi ambao wako katika kundi la wanyama walio katika hatari ya kutoweka hukadiriwa kuwa kati ya umri wa miaka 35 hadi 40

Aidha Faru Rajabu alizaliwa kwenye eneo la Ngorongoro mwaka 1979 hadi kufikia  mnamo mwaka 1993 alihama na kuhamia Serengeti.

Post a Comment

0 Comments