DENI LA SERIKALI LAFIKIA TSH.TRILIONI 64..52 KUTOKA TSH.TRILIONI 56.76.


📌RHODA SIMBA

IMEBAINISHWA kuwa hadi kufikia tarehe 30, Juni 2021 deni la Serikali lilikuwa Tsh.trilioni 64.52 ikilinganishwa na Tsh.trilioni 56.76 mwaka 2020.

Hayo yamesemwa leo April 12,2022 jijini Dodoma na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali [CAG] Charles Kichere wakati akizungumza na Waandishi wa Habari,baada ya kuwasilisha bungeni  ripoti za mdhibiti na mkaguzi  wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia mwezi Juni,30,2020/2021.

Aidha Kichere amesema licha ya kuongezeka kwa deni hilo lakini bado serikali ni himilivu.

Ukaguzi wa hesabu za serikali kuu umebaini mambo mbalimbali ikiwemo deni la Serikali la tilirion 64.52 na kwa kuzingatia kipimo cha deni la serikali la pato la taifa lakini bado ni himilivu

Aidha,Kichere amebainisha mapungufu ya udhibiti wa madai kwenye mfumo wa mfuko wa Bima ya Afya ambapo walibaini udanganyifu wa wanaume 56 walipata madai ya upasuaji wa kujifungua wakati huduma hizo hutolewa kwa wanawake.

Nilibaini kwamba madai 56 yanaonesha wanaume walipata huduma ya upasuaji au huduma za kawaida za kujifungua wakati huduma hizo hutolewa kwa wanawake

Kichere

Katika hatua nyingine Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali [CAG] Kichere amesema jumla ya taasisi 41 zililipa jumla ya Tsh.Bilioni 3.7 kwa wazabuni mbalimbali bila kudai risiti za kielektroniki kinyume na matakwa ya kanuni ya 28 kanuni ndogo ya kwanza ya kanuni za kodi kwenye mapato ya mwaka 2012.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali [PAC] Japhet Hasunga amesema mapungufu yaliyojitokeza wataenda kuyafanyia kazi wao kama kamati.

Ripoti ni nzuri na kuna hali nzuri inaoneshwa kwenye ripoti kwamba serikali ina watu wanafanya kazi lakini mwaka huu hakuna taasisi ambayo haijawasilisha ripoti na sisi kama kamati tutaenda kusimamia kuhakikisha kwenye kila sehemu penye mianya ya upotevu wa fedha ikae sawa

Hasunga

Hata hivyo Jumla ya ripoti za ukaguzi 20 zimewasilishwa kwa mwaka 2020/2021 zikiwa na jumla ya hati 999 za ukaguzi ambapo mamlaka za serikali za mitaa ni jumla ya hati ni 185 ,zinazoridhisha ni hati 178,hati zenye mashaka ni 6,na hati mbaya 1,serikali kuu ni jumla ya hati 308,hati zinazoridhisha 305, hati zenye mashaka ni 2,hati mbaya 1,mashirika ya umma kukiwa na jumla ya hati 195,hati zinazoridhisha 185,zenye mashaka 8 na kushindwa kutoa maoni hati 2 na miradi ya maendeleo kukiwa na jumla ya hati 292.

Post a Comment

0 Comments