📌DOTTO KWILASA

MRATIBU Ofisi ya Mufti wa Tanzania Mkoa wa Dodoma Swed Twaalib Swed amewataka Waislamu kote nchini kuwa kielelezo cha kujenga umoja wa kweli miongoni mwa watanzania ili kuweka alama ya amani na ushirikiano. 

Ameyasema hayo Jijini hapa wakati wa uzinduzi wa msikiti wa Chidachi-Miganga uliopewa jina la Al-Manaa ambao unasimamiwa na watu wa Misri ambao umetolewa kwa ajili ya marehemu Abdulaziz bin Muhsin wa Saud Arabia kama sadaka.

Msikiti huu umejengwa na Watoto wa Marehemu Abdulaziz bin Muhsin kama swadaka,mara nyingi watu hujenga misikiti kwa ajili marehemu wao kama sadaka na kusaidia wasiojiweza,hivyo ni muhimu kutoa sadaka

Aidha msikiti huo una uwezo wa kubeba waamini 800 kwa wakati mmoja kuwezesha kuswali na utatumika kwa wakazi wa Chidachi,Miganga na watu wanaoishi maeneo jirani.

Akizungumza katika uzinduzi huo, amesema uwepo wa msikiti huo utawajenga Watanzania kama ndugu na kuwa fundisho kwa watu wa eneo hilo na kutenda mema kama maagizo ya Mwenyezi Mungu yanavyotaka.

Msikiti huu uwaweke wakazi wa eneo hili pamoja na kuelewa kuwa tuna wajibu wa kumtanguliza Mungu katika maisha yetu yote, ukatoe pia mafunzo yatakayojenga umoja wa Watanzania, wale watakaoutumia wakaguswe kutekeleza maandiko matakatifu yaliyopo katika Quran

Mratibu huyo pia ametumia nafasi hiyo kumshukuru Mufti wa Tanzania kwa kukubali msikiti huo ujenge eneo hilo na kubainisha kuwa itakuwa kumbukumbu na alama ya kuenzi uhuru,amani na maelewano yaliyopo baina ya watanzania.

Pamoja na hayo amefafanua kuwa Msikiti huu sio rasmi bali upo ndani ya kampasi ya chuo ambacho kitafundisha watoto yatima kuanzia ngazi ya awali hadi sekondari,

 Mwishoo

Post a Comment

0 Comments