JESHI LA UHAMIAJI LAKAMATA RAIA WA ETHIOPIA WATANO MTERA.

 


📌RHODA SIMBA

JESHI la Uhamiaji Mkoani Dodoma linawashikilia watu watano ambao ni raia wa Ethiopia waliokamatwa katika kizuizi cha Mtera kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha Sheria na Taratibu. 

Kadhalika linamshikilia raia mmoja wa Tanzania Tito Mbwilo mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa Iringa na Tunduma ambaye alikuwa akisafirisha wahamiaji hao.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma Bahati Mwaifuge amesema kuwa wahamiaji hao haramu walikamatwa April 3 mwaka huu Kijiji Cha Mtera wakielekea Tunduma Mkoani Songwe.

Jeshi letu la uhamiaji tumefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu watano akiwemo Mtanzania mmoja wakisafirishwa kwenye gari yenye namba za usajiri T991 DXB Toyota Rumon ambalo lilikuwa linaendeshwa na Tito Mbwilo na huku akijua ni kosa 

Mbwilo


Aidha amesema baada ya kuwatia mbaroni wahamiaji haramu hao na dereva wao Tito Mbwilo alijaribu kutoroka bila mafanikio kutokana na umahili wa askari ambao waliweza kumdhibiti na kumuweka chini ya ulinzi.

Nitoe onyo kwa wasafirishaji wote wanaojihusisha na wahamiaji haramu katika Mkoa wa Dodoma kuacha mara Moja na kwamba jeshi tayari limebaini wamebadili mbinu kutoka magari makubwa na kutumia magari madogo

Niwaombe wananchi wote wakiwemo wakazi wa Mtera kuendelea na ushirikiano kutoa taarifa za kusafirisha wahamiaji haramu jambo ambalo litasaidia katika utendaji kazi wetu

 Mbwilo. 

Post a Comment

0 Comments