WAJASIRIAMALI WANAWAKE DODOMA WAFUNGUKA WAMSHUKURU RAIS SAMIA

 


📌WMJJWM

BAADHI ya Wajasiriamali Wanawake jijini Dodoma wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wajasirimali nchini kufanya kazi zao kwa tija na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

 Hayo yamebainika jijini Dodoma wakati wa ziara ya Menejimenti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na Naibu wake Amon Mapanju.

 Akizungumza na viongozi hao mmoja wa wajasirimali hao anayejishughulisha na uchakataji wa bidhaa za plastiki Aziza Abdi Hassir amesema kuwa aliamua kufanya shughuli hiyo kwa sababu ya kutaka kujiajiri na kufanya kazi ambayo itasaidia watu wengine wanapata ajira hasa wanawake.

 

Ameongeza kuwa kazi hiyo ameianza 2009 kwa kuanzisha kampuni ikiwa dampo na alijifunza kutoka kwa ndugu yake mkoani Dar Es Salaam na kuanza kupelekea chupa na bidhaa za plastiki kwa wanunuzi katika viwanda vikubwa mkoani Dar Es Salaam.

Amesema kuwa kwa sasa ana uwezo wa kupeleka tani 90 za chupa na bidhaa za plastiki katika viwanda ikiwemo chupa zenye soko mkoani Dar Es Salaam na plastiki zenye soko mkoani Dodoma katika viwanda mbalimbali.

Aidha Bi. Aziza amesema kuwa kwa sasa ana uwezo kuuza mzigo wa shillingi millioni  16 kwa kutokana mzigo wa tani 20 na pia wakiwa na uwezo wa kuzalisha kuzalisha tani 90 kwa wiki inayowawezesha kupata faida ya millioni 10 kwa wiki kutokana na biashara hiyo.

Mwanzoni hata mume wangu aliona aibu na kuwaza kwanini nifanye biashara hii ya chupa ila baada ya kuona mafanikio ameona faida yake na yeye sasa ndio amekuwa mfanya kazi mkubwa zaidi ya mimi
Bi. Aziza

Naye mume wa Bi. Aziza Abdi Hassir, Bw. Cirlo Chahai amesema kuwa wanawake wanakipewa fursa na kuaminiwa katika shughuli mbalimbali wanaweza kuleta mabadiliko na matokeo chanya hivyo jamii iwape fursa wanawake katika kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ili ziweze kuwakwamua kiuchumi na kuinua familia na jamii.

Kwa upande wake Bi. Hadija Zuberi ameiomba Serikali kuwatazama wajasiriamali kwa jicho la tatu hasa wanaojishughulisha na biashara ya chupa, bidhaa za plastiki na taka ngumu kwa kuanzisha viwanda vidogo na vikubwa ili waweze kupata soko kubwa la kupeleka malighafi zaidi, waweze kuongeza ajira na kipato.


 

Akizungumza katika ziara hiyo katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amesema nia ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kuyawezesha makundi maalum ikiwemo wajasariamali kama vile wamachinga kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kufanya biashara zao ndio maana ikaanzishwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makundi Maalum kutimiza mmoja ya lengo hilo.  

Tumekuja hapa kwa lengo la kujifunza na timu nzima ya Menejimenti ya Wizara pamoja na Naibu Katibu Mkuu wangu Amon Mpanju lengo tujue changamoto zinazowakabili wajasirimali na kuweka mikakati thabiti ya kusaidiana na Wizara za kisekta katika kutatua changamoto hizo
Dkt. Chaula  

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Amon Mpanju amewapongeza wanawake hao Bi. Aziza na Bi. Hadija kwa kuanzisha biashara hizo na kuweza kuwasaidia vijana kupata ajira zinazowasaidia kuendesha familia zao, hivyo kuwezesha watu wengi zaidi kupitia biashara hiyo.

Ameongeza kuwa Wizara imechukua maombi na changamoto zao na itahakikisha kushirikiana na Wizara za kisekta, kuzitatua changamoto hizo kwa manufaa ya wajasirimali katika kuendeleza shughuli zao ili waweze kupata manufaa zaidi.

Wakati huo Menejimenti ya Wizara hiyo ikiongozwa na Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula Imetembelea kikundi cha wajasirimali wanawake cha Five Dadaz kilichopo Nzuguni  jijini Dodoma kinachojishughulisha na biashara ya vitafunwa ikiwemo mikate keki na karanga.

 

Post a Comment

0 Comments