WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO WAKUMBUSHWA KULIPA MADENI

 


📌RHODA SIMBA

WATUMIAJI wa vyombo vya moto barabarani wametakiwa kuzingatia na kufuata sheria za usalama barabarani ikiwemo kulipa madeni wanayodaiwa bila kushurutishwa.

Hayo yamesemwa leo April 27,2022 Jijini Dodoma na Naibu Waziri ,Wizara ya Mambo ya Ndani Jumanne Sagini wakati akizindua Mashine mpya za kisasa za POS kwa ajili ya kukusunyia Maduhuli ya jeshi la polisi hususani kitengo cha usalama barabarani .

Amesema pia itatumika katika ununuzi wa silaha,Hati ya tabia njema na kukusanyia tozo mbalimbali barabarani hasa kwa madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani.

Sagini ameongeza kuwa Mashine hizo mpya zina tumia mfumo wa Android hivyo ina Wireless, inaskani leseni,inauwezo wa kuchukuwa alama za Vidole pamoja na kupiga picha jambo ambalo litasaidia kupunguza malalamiko ya wananchi yaliyokuwepo.

"Niwapongeza Jeshi la polisi nchini kwa kutumia wataalamu wake wa ndani kuendeleza mfumo huo ambao unakwenda kupunguzia jeshi hilo malalamiko na kuwafanya waweze kutekeleza majukumu yao bila kutumia nguvu kubwa kwa sababu mfumo huu kwa sasa unachukuwa taarifa za muhimu kwa Dereva hivyo hawezi kuja kukataa kwa sababu alama za vidole havifanani dunia nzima,"amesema.

Ninaimani mfumo huu utakwenda kuwa chanya kwenu na kwa wananchi hatutegemei kupata malalamiko tena ya kuwepo kwa makosa katika kumuandikia mtu kosa

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amewataka watumiaji wa barabara hususani madareva kutii sheria bila shuruti na kutoa ushirikiano pale Askari wa usalama barabarani wanapotaka kuchukua taarifa zao kwa ajili ya kujiridhisha wanapoandika ama kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto.


"Kwa mashine hizi mpya inahitaji dereva achukuliwe alama za vidole,picha na kuskani leseni sasa niwaombe usiwe mbishi pale askari anapotaka taarifa hizi mtoe ushirikiano kikubwa tii sheria bila kushurutishwa"Amesema IGP Sirro.

Naye Mkuu wa kitengo cha TEHAMA (ICT) wa jeshi la polisi nchini ACP Dawson Msongaleli amesema kuwa mfumo huo ulianza kwa kufanyiwa majaribia kwa mkoa wa Dar-es-salaam na Pwani mwaka 2017 baada ya kufanya kazi vizuri ndipo 2018 wakaanza kutumia kwa mikoa yote ya Tanzania Bara.

Amemaliza kuwa nia ya kutumia mashine hizi ni kuondokana na ule mfumo wa kujazana katika vituo vya polisi na kusababisha foleni isiyokuwa na maana na badala yake kila kitu kitafanyika kielektroniki.

 

Post a Comment

0 Comments