ZAIDI YA WATU MILIONI MOJA WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI NA MAGOJWA YATOKANAYO NA KAZI

 

📌SAIDA ISSA

SERIKALI imesema makadirio ya shirika la kazi na shirika la afya duniani mwaka 2016, zinaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni moja walipoteza maisha kufuatia ajali na magonjwa yatokanayo na kazi, huku ikiwataka waajiri kuheshimu haki ya usalama wa afya mahala pa kazi, kwa lazima na sio hiyari.

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Prof.Joyce Ndalichako aliyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa mahadhimisho ya siku ya afya mahala pa kazi ambayo huadhimishwa kila mwaka.

Waziri Ndalichako amesema kuwa kila mwajiri anatakiwa kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wake muda wote awapo kazini.

Hii sio hiyari kila mwajiri anatakiwa kuhakikisha Wafanyakazi wao wanakuwa salama muda wote wawapo kazini kwa kulinda na kuweka mazingira rafiki mahala pa kazi.
Prof.Ndalichako

Aidha amewataka waajiri na wamiliki wa maeneo ya kazi kuboreshe mazingira ya afya kwa namna ya kudhibiti viashiashiria vya ajali kazini, licha ya ufanisi wa zoezi hilo kuwa gumu kwa baadhi ya maeneo.

Naye mkuu wa Idara ya Ulinzi,usalama na muendelezo wa biashara katika banki ya CRDB Misina Alex amesema banki ya CRDB imekuwa na utaratibu wa kutoa huduma kwa wateja na kuhakikisha wafanyakazi wao wawapo katika maeneo yao ya kazi wanakuwa salama na afya ili waweze kuendelea kutoa huduma.

Aidha amesema kuwa wafanyakazi ni muhimu kutambua kuwa kila mtu usalama wake ni muhimu katika maeneo ya kazi na vyema kulinda afya.

CRDB ambayo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa makundi maalum na watu wote wenye mahitaji ili kuahikisha wanalinda usalama mahala pa kazi.

CRDB tumekuwa tukitoa huduma mbalimbali kwa vikundi kama wamama wajane,yatima na watu wote wenye mahitaji tumekuwa tukiwasaidia Ili kuhakikisha tunaunga mkono juhudi za usalama mahala pa kazi
Misina Alex

Mkurugenzi msaidizi wa kampuni ya Hopeca Daniel Manimba ameeleza kuwa Usalama mahala pa kazi ni jambo muhimu na wao kwa kulitambua hilo wamekuwa wakihakikisha usalama mahala pa kazi ni kipaumbele.

Amesema Hopeca kwa kulinda afya za watanzania imekuwa ikiandaa lishe ambayo imethibitishwa na TBS kwaajili ya kulinda afya za watumiaji.

"Lishe tunayoizalisha sisi kama Hopeca tumekuwa msitari wa mbele kuweka virutubisho katika unga tunaotengeneza kwani umekuwa ukisaidia kuimarisha afya,"amesema.

Usalama mahala pa kazi ni jambo muhimu kwa Kila taasisi, Hopeca imekuwa ikihakikisha hilo ndio maana tumeona tufike hapa kwajili ya kupata Elimu zaidi,"ameeleza.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii katika Mgodi wa  Barrick Bulyankulu Mary Lupamba amesema kuwa katika Mgodi wao suala la usalama mahala pa kazi ni jambo ambalo wamekuwa wakulipa kipaumbele kutokana na kuwa na mitambo mingi katika utendaji wao wa kazi.

Barrick tunawashukuru OSHA kuweza kuandaa maonesho haya mahiri ambayo yameweza kuyukutanisha na kutuweka karibu zaidi na Serikali
Mary Lupamba,

Aidha amesema kuwa maonesho hayo yameweza kuwasaidia wao kukutana na taasisi mbalimbali katika utoaji huduma na kubadilishana ujuzi na majarajio yao ni kuweza kukutana na wadau wengi zaidi.

Amesema mgodi wa Barrick unafanyakazi kwa kushirikiana na Serikali kupitia wizara ya madini kwani katika utendani wizara imekuwa ikiwa karibu sana kwa kuhakikisha kazi zinakwenda.

Naye Mganga Mkuu wa mgodi wa North Mara Gold Mine Dkt. Nicholas Mboya amesema kuwa mgodi una miaka Zaidi ya 15 tangu umeanza uchimbaji wa madini ya dhahabu na katika kipindi chote hicho mgodi huo umezingatia suala la afya kwa wafanyakazi kwa kuweka mifumo ya upatikanaji wa huduma za afya.

Mgodi wa Barrick umetengeneza mifumo ya kuhakikisha kwamba kila mfanyakazi aliyepo katika mgodi huu anapata huduma za afya na kulindwa kila muda kutokana na kuwepo kwa mitambo mbalimbali

Aidha amesema kuwa Serikali kupitia sheria mpya ya madini imefanya kazi kubwa kwa kuyatambua na kusaidia makampuni ya makampuni binafsi ya uchimbaji wa madini.

‘’Bunge letu limekuwa likitunga sheria Madhubuti na kuwapa miongozo kwa wamiliki wa migodi kutokana na sheria zilizowekwa na nchi kwa kufuata miongozo hiyo,’’ameeleza.

Maadhimisho hayo yamewahusisha kampuni na taasisi mbalimbali kutoka sekta binafsi na umma yakilenga kuonesha hatua na mafanikio waliyofikia kuimarisha usalama wa afya kwenye maeneo yao ya kazi.

April 28 kila mwaka Dunia uadhimisha siku ya afya mahali pa kazi, na lengo kuu likiwa ni kuhamasisha usalama wa mazingira na afya katika maeneo ya kazi.

Post a Comment

0 Comments