MAENDELEO YA JAMII KUWA TAALUMA KAMILI

 


📌MJJWM


WATAALAM wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, wametakiwa kuifanya taaluma hiyo kuwa taaluma kamili inayotambulika kisheria.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima wakati akiongea na Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ambao Waziri Gwajima Mei 06, 2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA).

Dkt. Gwajima alisema uwepo wa Sheria ya kuundwa kwa Taaluma ya Maendeleo ya Jamii itasaidia Taaluma ya Maendeleo ya Jamii kuwa na nguvu kwenye utekelezaji wa majukumu yao katika Mikoa Halmashauri.

Ameongeza kuwa changamoto wanazopitia Watalaam wa Maendeleo ya Jamii ikiwepo watu wasio wanataaluma kupangiwa majukumu ya Maendeleo ya Jamii hivyo uwepo wa Sheria itasaidia kutatua changamoto hizo zilizopo.

Taaluma ya Maendeleo ya Jamii lazima uwe kwamujinj Sheria ikawa na Bodi na Mamalka yake itasaidia kutatua changamoto nyingi zianawakabiki wataalam hawa na jamii yetu pia
Dkt Gwajima

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Zainab Chaula alisema Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wanapaswa kuwa chachu ya maendeleo na mabadiliko ya fikrsa na kusaidia Jamii kutatua changamoto zinazowakabili kwa kuwapa ufumbuzi na namna ya kukabiliana nazo.

Ukipita katika mitaa huko tunaona watu wengi wanapambana maisha hasa Wanawake hao ndio wetu tuwasaidie kutatua changamoto zao ili wajikwamie kiuchumi
Dkt Chaula

Naye rais wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) Angela Mvaa ameshukuru Waziri Dkt. Gwajima kwa nasaha na maelekezo yake na Chama hicho kitahakikisha kianweka nguvu ya kuwa na sheria ambayo itabadilisha kabisa mtazamo na uelekea wa Taaluma ya Maendeleo ya Jamii nchini.

Wakati huo huo Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima amekutana na kuzungumza na Chama cha Wataalam wa Ustawi wa Jamii nchini waliofika ofisini kwake kujadiliana namna ya kuboresha kada hiyo katika kuisadia jamii kupambana na changamoto mbalimbali.

 

Post a Comment

0 Comments